WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana,akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru kabla ya kuanza kupanda miti katika kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana,akisalimiana na wanafunzi pamoja na wananchi kabla ya kuanza kupanda miti katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana, akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana,akiwasaidia Wanafunzi kuweka udongo wakati wakipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Abdallah Mitawi, akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga,akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri,akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Diwani wa kata ya Ipagala Mhe.Dotto Gombo,akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew Komba, akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru,akipanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk. Pindi Chana,akizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Abdallah Mitawi, akizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu .
Diwani wa kata ya Ipagala Mhe.Dotto Gombo,akizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti Katika Eneo la Swaswa Bwawani kata ya Ipagala jijini Dodoma leo Januari 11, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59, ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwaka huu.
…………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Balozi Dk.Pindi Chana,amepiga marufuku uingizaji wa mifugo kwenye hifadhi za misitu na maeneo mbalimbali yaliyopandwa miti ili kuepuka uharibifu wa mazingira nchini.
Marufuku hiyo imetolewa leo Januari 11,2023 wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Swaswa Kata ya Ipagala jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar yatakayofanyika Januari 12, mwaka huu.
Dkt.Chana amesema kuwa, uharibifu wa mazingira unasababishwa na wananchi kuingiza mifugo yao katika hifadhi za Misitu.
“Tuanatakiwa kuilinda na kuitunza misitu kwa sheria zetu ni marufuku mtu yeyote kuingiza mifugo katika misitu hii tuliyonayo ili tuilinde itupatie mvua na kuondokana na athari za mabadiliko tabianchi”amesema Dkt.Chana
Amesema kuwa kama watu watandelea kuharibu mazingira ukame utaendelea kuisumbua nchi na kushindwa kufikia malengo yake ambayo imejiwekea katika miradi mbalimbali.
“Hata bwawa la kufua umeme la mto rufiji kupitia mradi wa Mwalimu Nyerere tutashinda kulijaza maji kama ambavyo tumejiwekea kwakuwa hatutakuwa na mvua za kutosha za kujaza maji katika mradi huu”ameeleza
Aidha amepiga marufuku tabia ya wakulima nchini kuandaa mashamba kwa kuchoma moto badala yake watumie njia mbadala ili kuendelea kutunza hifadhi Misitu.
“Uchomaji moto misitu siyo jambo sahihi wananchi tunapaswa kutafuta namana nyingine ya kuandaa mashamba siyo kuchoma moto kwakuwa tunaathiri sana misitu yetu ambayo inantupatia mvua na kuondokana na ukame ambao umekuwa ukitutesa katika sekta ya maji na umeme”amesema
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Abdallah Mitawi,a mesema kuwa katika madhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wanatarajia kupata miti 5,300 kwa muda wa siku tatu zilizopangwa.
Naye Diwani wa Kata ya Ipagala, Gombo Dotto amesema kuwa Mtu atakayeingiza mifugo yake katika eneo ilipopandwa miti asahau kupata mifugo yake kwani itakamatwa na sheria itafuata mkondo wake .