NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua kongamano lililoandaliwa na Red Cross lenye lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya akili lililofanyika leo Januari 7,2023 mjini Morogoro.
Rais wa Red Cross Tanzania David Kihenzile,akitoa taarifa wakati wa kongamano lililoandaliwa na Red Cross lenye lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya akili lililofanyika leo Januari 7,2023 mjini Morogoro.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kongamano lililoandaliwa na Red Cross lenye lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya akili lililofanyika leo Januari 7,2023 mjini Morogoro.
……………………………………….
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi ameagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) na Kamati ya Maafa nchini, kushirikiana na Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TCRS) katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mhe.Katambi amesisitiza kuwa Sheria ya Usimamizi wa Maafa inautambua ushiriki wa Red Cross katika Menejimenti ya Maafa nchini, hivyo ameelekeza Kamati ya Maafa kuendelea kushirikiana na Red Cross katika shughuli za usimamizi wa Maafa nchini.
Mhe.Katambi ameyasema hayo mjini Morogoro leo Januari 7, 2023 alipofungua kongamano liloandaliwa na Red Cross lenye lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya akili na fursa mbalimbali zinazopatikana kwa wadau ikiwemo SIDO, SUGECO na CASS – Track ili kuwasogeza vijana mbele kiuchumi.
Amesema sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 na Kanuni zake zinaelekeza maeneo ya kazi lazima yawe yanatoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi, hivyo ushirikiano wa OSHA na Red Cross utaimarisha Usalama na Afya mahali pa Kazi.
Aidha, ametoa rai kwa vijana wakiwamo wa Msalaba Mwekundu kutumia fursa ya mafunzo tarajali yanayotolewa na serikali kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira (Taesa) kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa uzoefu wa kazi.
Miongoni mwa mambo ambayo serikali imeyafanya Kwa vijana ni pamoja na miradi 85 ya vijana imepata mikopo, vijana 96,567 wamenufaika na Program ya Kukuza Ujuzi nchini na wengine 554 wamepatiwa mafunzo maalum kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi nje ya nchi.