Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari Iringa kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kurusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari Iringa kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kurusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
CHAMA cha mapinduzi (CCM),mkoani Iringa kimepongeza hatua ya Rais wa jamuhuri ya Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ruhusa ya kufanyika kwa mikutano ya kisiasa yenye ustaarabu kwa maslahi ya taifa
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Daudi Yassin amesema kuwa wanampongeza Rais Samia kwa ruhusa mikutano hiyo huku wakitarajia siasa safi na zisizo na uvunjifu w amani
“Sisi kama chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa tunampongeza dkt. Samia Suluhu Hassan kwa tamko alilolitoa ya kuruhusu vyama vya kisiasa na tufanye siasa za kistaarabu na zenye kujenga” alisema Yassin
Alisema kuwa wamejipanga vizuri kutoka matawi,kata ,wilaya hadi mkoa katika kufanya siasa safi na hawatarajii kuona uvunjifu wa amani ukifanyika kutokana na mikutno ya kisiasa .
Kwa upande wao wenyeviti wa CCM katika wilaya zote mkoani Iringa walisema kuwa pamoja na kuwepo kwa tetesi za mikutano yenye uwazi hawana wasiwasi badala yake wanatarajia mabadiliko makubwa na utenda kazi mzuri katika kipindi hiki
“Mheshimiwa mwenyekiti katika wilaya zetu hakuna wasiwasi wala mitetmo tupo vizuri na tupo tayari kufny siasa safi pamoja na kuwepo kwa baadhi ya maneno yanayotaka kututia wasiwasi nataka nikudhihirishie ya kwamba tupo vizuri”
Kwa upande wake chifu wa wahehe Mkoa wa Iringa Adam Sapi alisema kuwa yupo tayari kushirikiana na vyama vyote vya kisiasa hivyo ni vyema zikafanyika siasa safi zenye kuleta tija katika jamii .
“Kutokana na kauli aliyoitoa mama samia kuhusu ruhusa ya kufanya mikutano hapa nchini tupo tayari na tutashikana mikono na vyama vyot ili tuu tulete amani katika nchi yetu asante”
Nao wananchi wa manispaa ya Iringa wammpongeza Rais Dkt.Samia ambapo wamesema kuwa ruhusa hiyo itaonyesha ukomavu wa kisiasa pamoja na kusaidia kuibuliwa kwa changamoto nyingine zilizojificha kupitia vyama vya kisiasa .