Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-
- Amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa – Muhimbili. Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
- Amemteua Bw. Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC). Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).
- Amemteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
- Amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw. Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.
- Amemteua Bi. Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. Bi. Abdallah ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy nchini Geneva. Aidha, Bi. Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.
- Amemteua Bw. David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). Bw. Kafulila ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mstaafu.
Teuzi hizi zinaanza mara moja.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu