Nahodha wa timu ya Ihefu fc akikabidhiwa kombe la mashindano ya misitu sports Bonanza lilioandaliwa na uongozi wa shamba la miti la Sao Hill mkoni Iringa.
Mchezaji wa timu ya sawala akipokea medani baada ya kuibuka mshindi wa pili katika Bonanza lilioandaliwa na uongozi wa shamba la miti la Sao Hill wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
TIMU ya Ihefu FC imefanikiwa kutwaa kombe la mashindano ya misitu sports bonanza baada ya kuifunga timu ya Sawala FC kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika viwanja vya Makao makuu ya shamba la Sao Hill wilayani Mufindi.
Akizungumza Mara baada ya fainali hiyo mratibu wa mashindano ya misitu sports bonanza, Frank Milanzi alisema kuwa bonaza hilo lilizikutanisha Tarafa nne zinazolinguka shamba la miti la Sao Hill kwa kuwa na jumla ya timu 32 ambazo zilipambana ambapo Ihefu FC inaibuka kuwa bingwa.
Milanzi alisema kuwa mshindi wa kwanza wa bonanza kwa upande wa mpira wa miguu amepata kiasi cha shilingi laki tano, mshindi wa pili Laki tatu, mshindi wa tatu amepata kiasi cha shilingi laki mbili na mshindi wa nne amepata mpira hiyo yote kwa ajili ya kujenga ujirani mwema katika ya wananchi na shamba la miti la Sao Hill Mufindi.
Alisema kuwa mashindano ya misitu sports bonanza mwaka huu yamekuwa na msisimko tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma hiyo inatokana na maboresho ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara na kuongeza kwa ubunifu wa waandaaji wa bonanza hilo kila mwaka.
Milanzi alimazia kwa kusema kuwa mashindano ya misitu sports bonanza limesaidia kuongeza ujirani mwema katika kuhakikisha wananchi wanalinda shamba la miti la Sao Hill dhidi ya majanga ya moto pamoja wananchi kuhamasika kuendelea kupata miti kila wakati.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mpira Wilaya ya Mufindi Festo Kilipamwambu amewapongeza Uongozi wa TFS kwa kuendelea kuandaa Bonanza hili kila mwaka kwani linasaidia katika kujenga na kuimarisha umoja kati ya shamba na vijiji hivyo.
“Mashindano haya ya Misitu Sports Bonanza yamekua yakileta tija sana katika wilaya yetu ya Mufindi hususani katika timu zetu zinazozunguka wilaya na yamekua ni mashindano ya muhimu sana kwani yanasaidia katika kuibua vipaji na kuendeleza ujirani mwema baina ya watu mbalimbali” Alisema Festo
Kilipamwambu alisema kuwa anazipongeza timu zote zilizoweza kushiriki katika mashindano hayo na kuwapongeza mabingwa Ihefu FC kwa kutwaa kombe pamoja na washindi wa michezo mingine.
Alisema kuwa lengo mashindano hayo ni kuwambusha jinsi ya kuweza kuhifadhi rasilimali za misitu ikiwemo kupanda miti hasa katika kipindi hiki cha mvua na kuitunza pia kwa kushirikiana na jamii inayotuzunguka tunaweza kulinda na kuitunza misitu yetu.
michezo mbalimbali imechezwa na washindi kupewa zawadi zao ambapo IHEFU FC wakiibuka mabingwa wa mwaka huu na kutwaa kombe.