Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana na watoto yatima iliyofanyika kwa hisani ya Rock Solutions.
Mkurugenzi wa Rock Solutions Zacharia Elias Nzuki akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana na watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Msikiti wa Mkoa wa Mwanza Abubakar Zuberi uliopo kwenye Mtaa wa Mbugani Kata ya Mbugani Wilaya ya Nyamagana.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke (mwenye koti jeusi) Mkurugenzi wa Rock Solutions Zacharia Elias Nzuki pamoja na watoto wakila chakula
……………………………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jamii imetakiwa kuwathamini watoto yatima kwakuwapa mahitaji muhimu kama elimu,maladhi,chakula na mavazi ili waweze kutimiza ndoto zao
Rai hiyo imetolewa jana Januari 2, 2023 na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana na watoto yatima iliyofanyika katika viwanja vya Msikiti wa Abubakar Zuberi uliopo Mtaa wa Mbugani,Kata ya Mbugani Wilaya ya Nyamagana kwa hisani ya Rock Solutions Limited.
Alisema watoto yatima wanastaili kupata haki zao za msingi kama ilivyo kwa wengine kwani kwakufanya hivyo inawapunguzia mawazo ya kuwawaza wazazi wao waliotangulia mbele ya haki
Sheikh Kabeke amewakumbusha waumini wa dini zote kujenga tabia ya kuwasaidia watoto yatima huku akiwaonya baadhi ya watu ambao wanatabia ya kuwafanyia vitendo vya ukatili watoto hao kwani na wao wanastaili kupendwa.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Rock Solutions Zacharia Nzuki, alisema pamoja na changamoto wanazopitia watoto hao kwa kukosa wazazi hali hiyo haiwaondolei hadhi ya kuwa watoto wema wenye uwezo wa kuishi kwa upendo na heshima.
Alisema watoto yatima wamekuwa sehemu ya maisha yake hivyo Kila mwaka amekuwa akitoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao.
Akizungumza kwaniaba ya wazazi Amina Masenza, amewaomba watoto hao waishi kwa kufuata maadili mema wanayopewa na walezi wao ili waweze kuepukana na marafiki ambao wanaweza kuwafundisha tabia mbaya