Na.Joctan Agustino,NJOMBE
Vikosi kutoka idara tofauti za jeshi la Polisi mkoa wa Njombe vikiwa na siraha vimefanya operesheni katika miji na maeneo muhimu yenye mikusanyiko mikubwa ya watu Lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanakuwa Salama dhidi ya uhalifu na Mali zao hazidokolewi na vibaka .
Maeneo ambayo yametiliwa mkazi na kuwa na idadi kubwa ya Askari ni pamoja na maeneo ya masoko,makanisa,misikiti pamoja na maeneo ya mpakani wilayani Ludewa ambako ni wilaya inayopakana na Malawi kupitia ziwa Nyasa.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema jeshi limejipanga vywema kudhibiti kila aina ya uhalifu mkoani humo ili wananchi washereke mwaka mpya kwa amanj na kwamba ataethubutu kufanya KITENDO kiovu atajikuta hatiani kabla ya kufikia Lengo lake