Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali, Suleiman Mzee(wa tatu toka kushoto) leo Desemba 30, 2022 amekagua ujenzi wa shule mpya ya Sanzate Wilayani Bunda iliyoanzishwa ujenzi na Wananchi kupitia Mfuko wa Maendeleo wa jamii ya Ikizu(ICDT). RC Mara amesisitiza ujenzi unaozingatia ubora wa majengo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali, Suleiman Mzee leo Desemba 30, 2022 akikagua ujenzi wa shule mpya ya Sanzate Wilayani Bunda. Pichani akiwa ameshika pima maji kuona kama ujenzi huo unazingatia vipimo husika.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali, Suleiman Mzee leo Desemba 30, 2022 akisaini Kitabu cha wageni kabla ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sanzate Wilayani Bunda iliyoanzishwa ujenzi na Wananchi kupitia Mfuko wa Maendeleo wa jamii ya Ikizu(ICDT).
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Shule mpya ya Sanzate iliyopo wilayani Bunda ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi huo