Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akioneshwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Filbert Mponzi (kulia) namna wananchi watakavyoweza kutumia huduma ya ukadiriaji na ulipaji kodi na tozo za sekta ya ardhi kupitia mawakala wa Benki hiyo wakati wa uzinduzi wa mkakati maalum wa ushirikiano wa wizara ya ardhi na Benki ya NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 20,2022.