********************
NA FARIDA MANGUBE. MOROGORO
Wanafunzi zaidi ya 300 wa vijiji vitatu vya Kitange One, Kitange Two pamoja na kijiji cha Usungu kata ya Mtumbatu wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wanahatarisha maisha yao kwa kulazimika kutembea umbali wa kilometa 36 kila siku kwenda shule ya sekondari Mtubatu na kurudi nyumbani huku baadhi ya wanafunzi wa kike wanaoishi kwenye vibanda vya kupangisha maarufu kama magetu wakipachikwa mimba na wanafunzi wa kiume wakitumbukia kwenye tatizo la dawa za kulevya.
Hali hiyo ilelezwa na wazazi na walezi wa wanafunzi hao walipokuwa wakijitolea kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari kwa lengo la kuwasaidia watoto wao kuondokana na changamoto zinazowakabili zikiwemo kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni.
mzee maarufu katika kijiji cha Kitange bwana Charles Mawaya alisema kuwa tangu Tanzania ipate huru watoto wao wamekuwa wakiteseka na hivyo kusababisha wanafunzi kushindwa kufaulu katika masomo yao hali inayosababisha vijiji hivyo kutokuwa na watu wasomi waanaoweza kuwaletea maendeleo.
“kijiji chetu hakina watu wasomi kutokana na kutokuwa na miundombinu bora ya elimu na maisha magumu waliyonayo wazazi kwa kushindwa kuwakodishia vyumba watoto wao karibu na shule, lakini pia wawzazi wengi tumekuwa hatuna muamko juu ya elimu ivyo tukajikuta hatuna wasomi kabisa kwenye kijiji chetu ndio maana leo tumeamua kuanza ujenzi wa shule yetu kwa kutumia rasilimali ndogo tulizonazo” alisema mzee charles.
Diwani wa kata ya Tumbatu bwana Moses Sewando ameeleza madhara yanayokana na vijiji hivyo kukosa shule ya sekondari na adha wanayoipata wanafunzi huku akiwashuku wadau waliojitokeza kuchangia fesdha na vifaa kwa ajili ya shule hiyo.
“Nawashukuru sana wadau wetu akiwemo mbunge wetu wa jimbo la kilosa mheshimiwa Paramagamba Kabudi kwa kuchangia mifuko 200 ya saluji, mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kilosa kwa kutuchangia mifuko 5o pamojana name nimechangia mifuko 70 ili kusukuma haraka zoezi la kuanza ujenzi wa shule hii” alisema Moses.
Aidha wananchi wa vijiji hivyo wanatamani kuona ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwaa wakati na ikiwezekana mwezi januari mwaka 2023 wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo endapo serikali itawaunga mkono mapema kwa kuwawezesha vifaa muhimu vitakavyosaidia kumalizia ujenzi wa shule hiyo.
Hata hivyo Serikali imekuwa ikihimiza wananchi kuibua miradi mbalimbali katika maeneo yao kulingaana na mahitaji yao kwa awakati huo na kwambaada ya kuanzisha mradi huo serikali kupitia halmashauri imekuwa ikiwasaidia wananchi hao kwa kumalizia ujenzi huo ambapo hadi sasa wananchi hao awamekaamilisha hatua ya kwanza ya kufyatua tofaali pamoja na uchimbaji wa amsingi tayari kwa kuanza ujenzi.