Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Maharage Chande kuhusiana na Kituo cha kusafirishia umeme (Switchyard) katika Mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) katika Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
(PICHA IKULU NA JOHN BUKUKU-RUFIJI)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Maharage Chande kuhusiana na jengo la Mitambo (Power House) kwenye Mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere JNHPP katika Mto Rufiji tarehe 22 Desemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wananchi wa Mikoa ya Pwani na Morogoro kabla ya kuzindua Shughuli ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022.
Kutoka kushoto ni Mkuu wamkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, Fatma Mwassa Mkuu wa mkoa wa Morogoro na Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ambao pia walihudhuria katika hafla ya Kufunga Njia ya Kuchepusha Maji na Kuanza Ujazaji wa Maji kwenye Bwawa la Kuzalisha Umeme (Megawati 2115) la Julius Nyerere (JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani tarehe 22 Desemba, 2022 ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro alipewa nafasi ya kuzungumza.
**********************
Na Selemani Msuya, Rufiji
WAKUU wa mikoa ya Pwani na Morogoro wamesema wamejipanga kuhakikisha umeme utakaozalishwa kupitia Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), unachochea shughuli za maendeleo na kijamii kwa wananchi wao.
Pia viongozi hao wameahidi kuulinda na kuutunza mradi utakaozalisha megawati 2,115, ambao unagharimu zaidi ya Sh.trilioni 6.5 ili uweze kuwa endelevu.
Akizungumza wakati wa zoezi la kujaza maji kwenye bwawa hilo lililofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan leo katika eneo la mradi wilayani Rufiji, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenga amesema ukamilifu wa mradi huo unaenda kichocheo shughuli za uzalishaji mkoani kwake.
Kunenga amesema mradi huo utawezesha umeme katika mkoa huo kupatikana kwa asilimia 100 hivyo kuongeza uzalishaji.
“Mheshimiwa Rais sisi Pwani tunashukuru bwawa hili la JNHPP kuwepo hapa Rufiji, tunaamini Watanzania watanufaika ila Pwani itanufaika zaidi, nikiahidi kwa kushirikiana na wenzetu wa Morogoro tutaulinda na kuutunza,”amesema.
Aidha, Kunenga amemuomba Rais kuangalia uwezekano wa kukamilisha ujenzi wa barabara kutoka Mwanarumango hadi kwenye mradi kwa kiwango cha lami, ili kurahisisha kufika eneo husika.
Mkuu huyo wa mkoa amesema barabara kutoka Kisarawe hadi JNHPP ni fupi na rahisi kufikika hivyo anamuomba Rais Samia kutenga bajeti ya ujenzi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa alisema ameomba ujenzi wa bwawa hilo uwe ni neema na kwa wananchi wa mkoa huo kwa kupatiwa huduma za afya, elimu na nyinginezo.
“Sisi tunaomba mradi huu ukianza tupate mgao kupitia CSR ili tuweze kujenga Hospitali ya Rufaa ya kisasa, chuo cha afya na mengine,” amesema.
Mwasa ameungana Kunenga katika kuhakikisha miradi huo inalindwa na kutunzwa.