Na Dotto Mwaibale, Singida.
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini Mwalimu Mussa Sima ametoa Sh. Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Unyianga iliyopo Manispaa ya Singida ambapo Serikali ilitoka Sh. 50 Milioni.
Ujenzi wa Zahanati hiyo umekwisha kamilika na tayari watumishi wawili wamekwisha fika ambao ni daktari na muuguzi.
Akizungumza wakati wa ziara yake aliyoifanya juzi Desemba 20, 2022 ya kukagua miradi ya maendeleo Sima alisema Serikali umefanywa kazi kubwa katika jimbo kwa kutoa Fedha nyingi.
Miradi aliyoitembelea na kuikagua ni ujenzi wa Shule ya Sekondari katika kata hiyo, ujenzi wa madarasa mawili shule ya Msingi ambapo alichangia Sh. 2 Milioni na kukagua ujenzi wa barabara za Kindai-Unyianga inayojengwa sambamba na madaraja na kunyanyua tuta barabara ya Unyianga Mwankoko.
Alisema barabara hiyo imekamilika baada ya Serikali Kuu kutoa Sh.370 Milioni fedha ambazo zimechagiza kuchochomea kasi ya maendeleo katika jimbo hilo.
Katika hatua nyingine Mbunge Sima alipata fursa ya kuzungumza na baraza la wa wazee wa kata hiyo sanjari na kula nao chakula.
Aisha Sima alizungumza na makundi ya wauza kahawa na vikundi vya akina mama na kukiunga mkono kwa kukipa Sh 120, 000 na kikundi cha wauza kahawa Sh 70, 000 na kuwapongeza kwa umoja wao.
Katika ziara hiyo Mbunge Sima aliongozana na Diwani wa Kata ya Unyianga, Geofrey Mdama ambapo alitumia nafasi hiyokumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo.Mbunge Sima akitoa mchango kuwaunga mkono wauzaji wa Kahawa wakati wa ziara hiyo.