Y9 Microfinance imezindua matawi mapya matano jijini Dar es Salaam ili kuimarisha utoaji wa huduma, huku
ikilenga kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Matawi hayo yaliyopo maeneo ya Makumbusho, Mbezi Luis, Tandika, Kigamboni na Buguruni yatawezesha wateja kupata huduma za mikopo kwa urahisi zaidi.
Y9 imekusudia kuongeza urahisishaji kwa wateja ambao hawawezi kumudu ununuzi wa mara moja wa simu janja na wanatafuta njia za mbadala za mkopo wa simu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Y9, Faith Pella alisema hatua hiyo ni mkakati wake wa kukuza biashara ya Y9 Microfinance kwa kupeleka huduma za mkopo wa simu janja
karibu na wateja wetu. Tunatoa huduma za mkopo wa simu janja za 4G kwa vikundi tofauti wakiwemo wafanyakazi, wajasiriamali na watu binafsi.
“Tunafuraha kuwataarifu wateja wetu kwamba, sasa wanaweza kupata huduma zetu kwa urahisi katika vituo vyetu vya Y9 kote jijini Dar es Salaam na tutaendelea kufungua katika mikoa mingi zaidi ili kuwafikia wateja wengi zaidi nchini,” Mkurugenzi Mtendaji wa Y9 alisema.
Y9 kushirikiana na Samsung tunatoa simu mahiri za bei nafuu na zenye ubora kwa Watanzania. Wateja sasa wanaweza kupata mkopo wa simu aina ya Samsung kwa urahisi kwa bei ya chini ya kianzio ya TZS 40,000 kupitia Y9 Microfinance na kurejeshakuanzia TZS 2,000 kwa siku kama marejeshoya mkopo, ” Mkurugenzi Mtendaji wa Y9 aliongeza.
“Tumeanza na mkopo wa simu janja, na tunamipango endelevu ya kuleta huduma zaidi ili kuwapa wateja wetu huduma bora za kifedha zitakazopatikana katika programu yetu ya Y9” aliendelea.
Y9 imejipanga kutoa ushirikishwaji wa kifedha kupitia huduma za kifedha za kidijitali ambazo zitaathiri maisha ya kijamii na kiuchumi ya watu wa Tanzania.
Kwa maelezo zaidi, mteja anaweza kupiga 0 800 75 0260 bila malipo na kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata huduma hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Y9 Microfinance Faith Pella akiwa sambamba na Mkuu wa Kitengo chaa Mauzo na Usambazaji Fredrick Mtui wakikata utepe ikiwa ni moja ya uzinduzi wa matawi
mapya matano ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, ili kuimarisha
utoaji wa huduma, huku ikilenga kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Y9 Microfinance Faith Pella alipokuwa akizungumza na Baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzindua moja ya tawi kati ya matawi
mapya matano ya taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, ili kuimarisha
utoaji wa huduma, huku ikilenga kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Mkuu wa Kitengo chaa Mauzo na Usambazaji wa Y9 Microfinance ,Fredrick Mtui akifafanua jambo kwa baadhi ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua moja ya tawi kati ya matawi
mapya matano ya taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, ili kuimarisha
utoaji wa huduma, huku ikilenga kuwafikia Watanzania wengi zaidi.