Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Vyumba vya madarasa 38 vilivyogharimu kiasi cha sh.Milioni760 katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani,vimekamilika .
Vyumba hivyo vina uwezo wa kubeba wanafunzi 1,900 kati ya 4,806 waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza 2023 ambapo vipo tayari kwa matumizi mara baada ya shule kufunguliwa Januari 2023.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mhandisi Mshamu Munde amewapongeza wote waliofanikisha ujenzi huo na kufanya ukamilike kwa wakati.
Aidha,Munde ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi Makini wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Elimu ili kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji.