Jumla ya vijana 300 kutoka vikundi 14 mkoani Iringa wamewezeshwa na Mradi wa Imarika kijana ulio chini ya Shirika lisilo la kiserikali la LYRA in Afrika kuzitambua fursa mbalimbali ufugaji kwa ajili ya kuwakomboa kimaisha na kuwasaidia kuliondoa kundi hilo kubwa kuishi maisha ya vijiweni.
Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembelea wafungaji mbalimbali waliofanikiwa mratibu wa mradi wa imarika kijana,Gift Mafue alisema kuwa jitihada zaidi za kuwawezesha vijana kutambua fursa na kujiajiri zinaitajika ili kuondosha kundi kubwa la vijana kusalia vijiweni na kujihusisha na vitendo viovu.
Mafue alisema kuwa wimbi la vijana wanaojihusisha na Uhalifu limechangiwa na changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na ufinyu wa maarifa ya utambuzi wa fursa za kujiajiri.
Alisema kuwa shirika la Lyra in Afrika kwa kutambua changamoto hiyo wamejikita katika uwezeshaji wa vijana katika wilaya ya Iringa na kilolo mkoani Iringa kutumia fursa zinazowazunguka ambapo sasa asilimia 81 ya vijana 1900 wamejiajiri
Mratibu huyo wa mradi wa Imarika kijana kutoka shirika la Lyra in Afrika alisema hii ni awamu ya pili uwezeshwaji wa vijana hao kutoka wilaya ya kilolo na Iringa.
Mafue alisema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuwainua vijana na kuimarisha uchumi wao kwa ujumla
Katika awamu hii ya pili ya mradi wa imarika kijana jumla ya vikundi 14 vimenufaika na moingoni mwao wamepata fursa ya kutembelea shughuli za mfugaji wa kuku wa asili, Nguruwe na kuku wa kisasa na ufugaji wa Nyuki katika maeneo mbalimbali ya mkoani Iringa
Hashim Deus na Rosemary Sanyagi ni vijana wanufaika katika ziara hiyo ya ujasiriamali walisema kuwa wanalishukuru shirika lisilo la kiserikali la LYRA in Afrika kwa kuwapatia fursa mbalimbali za kujifunza miradi ya ufugaji
Walisema kuwa wataitumia fursa hiyo kuhakikisha wanafuga kisasa na kufanikiwa kukuza uchumi wao binafsi na uchumi wa vikundi.
Naye Mwenyeji katika ziara hiyo,Hosea Mtewele ambaye ameeleza namna alivyoanza ufyugaji akiwa na kuku watano nah ii leo tunapozungumza akiwa na kuku zaidi ya efu tatu huku uzalishaji na biashara ikiwenelea kushika kasi na kuchoche kipato chake
Mtewele alisema kuwa analipongeza shirika la lyra in afrika katika kusaidia vijana kuwa ni hatua kubwa itakayochochea kasi ya maendeleo vijijini kwa kuwa vina vijana wengi watatambua fursa zilizopo katika maeneo yao na kuanzisha miradi itakayosisimua uchumi binafsi na wa kijiji kwa ujumla