Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe akikabidhi Tuzo katika hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kitaifa za Ubora kwa Washindi wa Msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe akikabidhi Tuzo katika hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kitaifa za Ubora kwa Washindi wa Msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe akizungumza katika Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kitaifa za Ubora kwa Washindi wa Msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza katika Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kitaifa za Ubora kwa Washindi wa Msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wadau wa viwango wakifuatilia kwa ukaribu hafla ya utoaji tuzo za kitaifa za ubora kwa washindi wa msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wadau wa viwango wakifuatilia kwa ukaribu hafla ya utoaji tuzo za kitaifa za ubora kwa washindi wa msimu wa 2022/2023 iliyofanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe (katikati) akipata picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Kitaifa za Ubora Washindi wa Msimu wa 2022/2023 leo hafla hiyo ambayo imefanyika leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
NAIBU Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe amesema Nchi za Afrika zimekua na kiwango kidogo cha biashara baina yake ukilinganisha na mabara mengine.
Takwimu zinaonesha Biashara baina ya nchi za Afrika ni 16.6% ya biashara zote za nje (exports) ukilinganisha na 68.1% baina ya nchi za ulaya, 59.4% baina ya nchi za Asia na 55.0% baina ya nchi za Amerika.
Ameyasema hayo leo Desemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Kitaifa za Ubora kwa Washindi wa Msimu wa 2022/2023 ambapo washindi wamekabidhiwa tuzo hizo na kuahidi kuendelea kuhamasisha uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora.
Mhe.Kigae amesema serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iliona umuhimu wa kuanzisha Tuzo za ubora za Kitaifa na kutoa jukumu la kuziratibu kwa Shirika la Viwango Tanzania pamoja na TPSF kwa kushirikiana na Taasisi nyingine.
“Tuzo hizi ni sehemu ya mipango ya serikali katika kuboresha huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini kupitia matumizi ya viwango na kanuni za ubora kwa taasisi za umma na sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa mifumo, bidhaa na huduma zinakidhi mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa na hivyo kufanya vizuri kwenye masoko ya ngazi zote hizo”. Amesema
Amesema Serikali imedhamiria kujenga msingi shindani na endelevu wa viwanda wenye kuwezesha biashara ulimwenguni kwa kuzingatia faida za mahali tulipo kijiografia na rasilimali zilizopo nchini kupitia sera, mikakati na mipango kwa mageuzi shirikishi ya viwanda.
Aidha amesema washindi wa tuzo za ubora kitaifa mwaka wa 2021/2022 walishiriki katika mashindano ya kikanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Quality Awards) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Quality Awards).
Pamoja na hayo amesema katika mashindano hayo makampuni kutoka Tanzania yalifanikiwa kunyakua tuzo kama ifuatavyo.
- EAC Best Large Company of the Year – Said Salim Bakhresa & Company Ltd
- EAC Best SME Product of the Year – Faima Products (Tanzania)
- EAC Services of the year (SMEs) – Caps Tanzania Ltd
Hata hivyo amesema miundombinu ya Ubora yaani Quality infrastructures ni moja kati ya maeneo muhimu yanayohitajika kuchangia ukuaji na maendeleo ya sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
“Matumizi ya Viwango, Udhibiti wa Ubora, ithibati pamoja na ugezi husaidia kulinda soko la bidhaa na huduma ndani ya nchi yetu na vilevile huboresha nafasi ya bidhaa na huduma zetu katika ushindani kwenye masoko ya kimataifa”. Ameeleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa kamati inayoratibu tuzo za Kitaifa za Ubora ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na hivyo kupelekea ukuaji wa tuzo hizi ukilinganisha na misismu miwili iliyopita.
Ameeleza kuwa wazalishaji na watoa huduma wanahitajika kujengewa au kujijengea utamaduni wa ubora na ushindani hapa nchini. Vilevile wanahitaji kufahamu uhusiano kati ya ubora na ushindani. Hii ndiyo njia pekee kwa nchi yetu kusonga mbele kibiashara.
Amesema maandalizi ya tuzo hizo yalifanyika kwa ushirikiano wa karibu na taasisi mbalimbali ikiwemo, TPSF, CTI, SIDO, ZBS, TWCC, TCCIA, TANTRADE, SMIDA, TPSF pamoja na taasisi nyingine.
Vilevile amesema mashindano ya tuzo kwa msimu wa mwaka 2022/2023 yamekua ni yenye muamko mkubwa kutoka kwa washiriki ambapo idadi ya washiriki kwenye kila kipengele imeongezeka isipokuwa ushiriki kwa makampuni madogo kwenye kipengele cha muuzaji bora wa bidhaa nje nchi.