NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, SAME
MKUU
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema uwekezaji kwenye eneo la
viwanda uliofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)
kwenye mkoa huo umeleta faraja kubwa kwa wananchi.
Mkuu
huyo wa Mkoa ameyasema hayo Desemba 14, 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukarabati
wa Kiwanda cha Kuchakata Tanagawizi cha Mamba Miamba Ginger Growers kilichoko
wilayani.
Kiwanda
hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Ushirika wa wakulima wa Tangazwizi
wa Mamba Miamba Ginger Growers ambapo PSSSF inamiliki asilimia 67% ya hisa na
wanaushirika wanamiliki asilimia 33%.
PSSSF
pia imewekeza kwenye kiwanda cha Kimataifa cha Biadha za Ngozi cha Kilimanjaro
“Mmetupa
heshima kubwa na mmetupa maendeleo makubwa kwenye mkoa wetu wa Kilimanjaro”
alisema Mhe. Babu.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwahimiza wakulima wa Tangawizi kutunza mioundombinu ya kiwanda
ili kwa pamoja ilete faida kwa wananchi.
Kwa
upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini PSSSF, Dkt. Aggrey Mulimuka
alisema, Bodi inaridhishwa na uwekezaji unaofanywa na Mfuko kwenye miradi
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Mamba Miamba.
“Wajibu
wetu ni kuhakikisha mradi huu na uwekezaji mwingine unaofanywa na Mfuko unakuwa
na manufaa kwa wananchama na bila mashaka yoyote tunaamini mradi huu utalipa.”
Alisema.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba alisema uwekezaji uliofanywa na
Mfuko huo unafanyika kwa kufuata miongozo ya Benki Kuu pamoja na Sera ya
Uwekezaji ya Mfuko.
“Lengo
kuu likiwa ni kuwa na uendelevu wa kifedha ili kulinda thamani ya fedha za
wanachama na lengo lingine ni kupata faida ya uwekezaji ili kukuza hazina na
kuongea uwezo wa kulipa Mafao pale yanapohitajika na pia kuchochea maendeleo ya
kijamii na kiuchumi katika nchi.”
Akizungumzia
ukarabati wa kiwanda hicho, CPA Kashimba alisema kiwanda hicho kilijengwa mwaka
2012 lengo likiwa ni kusindika tangawizi kiasi cha tani 9.8 kwa siku jambo
ambalo halikuwezekana na kiwanda kilizalisha chini ya tani moja kwa siku
kinyume na matarajio sababu kubwa ikiwa ni uwezo mdogo wa mitambo.
Kutokana
na sababu hiyo wanaushirika kupitia Mbunge wa jimbo la Same, Mhe. Anne Kilango
Malecela uliomba ubia na PSSSF na baada ya kufanyika uchambuzi Mfuko ulikubali
kuingia ubia na kuanza ukarabati wa majengo na ufungaji wa mashine mpya za
kisasa uliogharibu karibu shilingi Bilioni 2.
“Kiwanda
kina uwezo wa kuzalisha tani 10 kwa siku na kina maabara za kisasa zenye
kukidhi viwango vya kimataifa kwa kupima ubora wa tangawizi inayozalishwa
kiwandani.” Alifafanua CPA Kashimba.
Mbunge
w ajimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malecela ambaye ndiye alitoa wazo
la kuanzishwa kiwanda cha kuchakata Tangawizi katika eneo hilo aliishukuru
PSSSF kwa kukubali kuwekeza kwenye kiwanda hicho kwani wakulima watanufaika na
uwekezaji huo.
“Ninachoomba,
kiwanda tayari tunacho na kina mitambo ya kisasa, tunahitaji tuwe na umeme wa
uhakika, na mimi niombe Mkuu wa Mkoa Kiwanda kifungiwa transfoma yake ili
kijitegemee na hivyo itapunguza adha ya upatikanaji wa uhakika wa umeme.”
Aliomba Mhe. Anne Kilango Malecema.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Edward Mpogolo alisema kabla ya
uwekezaji huo soko la uhakika la Tangawizi lilikuwa na mashaka lakini mashaka
hayo sasa yameondoka kupitia uwekezaji huo wa PSSSF kwani soko la uhakika la
Tangawizi lipo.
“Ndugu
zetu wa PSSSF wametusaidia kuboresha zao la Tangawizi kwa kutuletea kiwanda na na
imani yetu kubwa sana wana Same na hususan sisi wakulima wa zao la Tangawizi
watatusaidia kutengeneza soko na kuboresha bei ya Tangawizi katika maeneo yetu
na Tanzania kwa ujumla.” Alisema Mhe. Mpogolo.
Naye mkulima wa kwanza wa zao la Tangawizi katika
kijiji cha Goha mahali ambapo kiwanda hicho kipo, Bw. Kilango Chikira Mfanga
alisema kiwanda hicho kimeleta faraja kubwa kwa wakulima yeye akiwemo.
“Niliingiza
mbegu ya Tangawizi kwenye eneo hili mwaka 1988 na niliweza kuuza maeneo
mbalimbali ya nchi ikiwemo Arusha, Moshi na Dar es Salaam na Tangawizi ya hapa
ni bora na inapendwa sana.” Alisema.