Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiangali picha za vivutio vya utalii vya Tanzania zilizowekwa kwenye wigo wa ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiwa katika mkutano na Viongozi wa Bodi ya Utalii na Utalii Tanzanzia (TTB).
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akisisitiza jambo wakati wa mkutano
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka ndani yakituo chakutolea taarifa wa utalii kidijitali cha Bodi ya Utalii na Utalii Tanzanzia (TTB).
………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasilina Utalii, Prof Eliamani Sedoyeka ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa juhudi wanazozifanya za kutangaza utalii wa Tanzania kupitia matukio mbalimbali yanayofanyika ndani na nje ya Tanzania.
Pongezi hizo amezitoa alipokutana na Menejimenti ya TTB wakati wa ziara yake ya leo 15/12/2022 katika ofisi za TTB jijini Dar es Salaam, ambapo ameweza kujua mikakati ya TTB ya kutangazaji utalii pamoja na changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao.
“Natarajia kuona mnaongeza ushirikiano na wadau wa utalii ili kwa pamoja muweze kuongeza wigo wa kupenya kwenye masoko mengine makubwa ya utalii, lazima kuwa wabunifu wa kuibua mbinu zenye kuleta tija ili tuweze kufikia lengo tuliojiwekea la kufikisha watalii Milioni 5 ifikapo mwaka 2025”. Alisema Prof Sedoyeka.
Aidha, Katibu Mkuu ametembelea kituo cha kutolea taarifa za utalii Kidijitali na kuishauri bodi kushirikiana na wadau wengine wanaosimamia maeneo ya Utalii ili waweze kupata taarifa sahihi za vivutio husika na baadaye kutumika katika shughuli mbalimbali za utangazaji.