Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora Mohamedi Shomari akiwa eneo la tukio wakati wakuzima moto katika barabara ya salimini manispaa ya Tabora Shuhuda Katika tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara jirani yake Matata Saidi Matata akizungumza katika tukio la moto. Watu mbalimbali waliojitokeza kuangali tukio hilo la moto ilolotokea leo asubuhi manispaa ya Tabora . Wananchi mbalimbali wakiwa jirani na duka lilopata ajali ya moto
*******************
Na Lucas Raphael,Tabora
Moto mkubwa umeteketeza mali mbalimbali za samani za dani ambazo hadi sasa thamani yake hajaweza kufahamika baada ya Maduka matatu ya wafanyabiashara yaliopa katika barabara ya Salimini Mkoani Tabora
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora Mohamedi Shomari alisema majira ya 4 na dakika kumi walipata wito wa tukio la Moto kwenye frem za Maduka.
Alisema kwamba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika kwenye tukio kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na Usalama , Jeshi la Ppolisi na Jeshi la Wananchi na walifaniiwa kulikabili tukio hilo .
Alisema Maduka matatu yaliteketea kwa moto na Stoo za kuhifadhia mali na baadhi ya samani ziliokolewa .
Kwa Upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao alisema kwamba mtu mmoja ambaye ni Mmiliki wa duka mojawapo alipopata taarifa alifika eneo la tukio na alidondoka chini na kupoteza fahamu.hivyo alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa Kitete.
Alisema kwamba jeshi la polisi kwa kushirikia na shirika la umeme Tanesco wanaendelea na uchunguzi wa kina kubaini nini chanzo cha moto huo .
Alisema mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo jeshi hilo litatoa taarifa kwa umma na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Nae Shuhuda Katika tukio hilo ambaye ni mfanyabiashara jirani yake Matata Saidi Matata akizungumza katika tukio hilo alisema kwamba litokea ghafla baada ya Mmiliki aliyeuguliwa duka Juma White akiwa ameingia ndani na kukuta tayari moto unawaka.
Alisema muda kidogo alitoka na kuita wafanyabiashara wenzake ili wakamsaidie .kuokoa vitu vilivyopo dukani ,Lakini wakamuona anakimbia kuchukua bodaboda ya pikipiki na kuelekea Ofisi ya Jeshi la Zima moto na Uokoaji kwenda kutoa taarifa.
Matata ambaye ni Shuhuda anaiomba Serikali kuongeza Magari ya Zima Moto na Uokoaji kwa sababu yangekuwepo mawili au matatu wangefanikiwa kuotoa vitu vingi.
Aidha alisema moto ulikuwa mkubwa ambao ulikuwa umetanda katika duka moja la Juma White ambapo ndio ulianza dukani kwake na kutambaa hadi maduka mengine mawili.