Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Magereza, Kaimu Kamishna wa Sheria na Utawala wa Magereza, George Mwambashi (kulia), akikabidhi nyaraka za ofisi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), Moremi Marwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, leo. Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Maduhu Kazi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, akizungumza katika kikao cha makabidhiano ya ofisi kati ya Kamishna Jenerali wa Magereza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) kilichofanyika jijini Dodoma
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), Moremi Marwa (kushoto), akisaini taarifa ya makabidhiano ya ofisi na Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Magereza, Kaimu Kamishna wa Sheria na Utawala wa Magereza, George Mwambashi (kulia), jijini Dodoma, leo Disemba 13, 2022. Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi (katikati), akimsikiliza Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Magereza, Kaimu Kamishna wa Sheria na Utawala wa Magereza, George Mwambashi, akizungumza katika Kikao cha makabidhiano ya ofisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), Moremi Marwa (wapili kushoto), jijini Dodoma,
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi (kulia), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), Moremi Marwa akizungumza katika Kikao cha makabidhiano ya ofisi na Kamishna Jenerali wa Magereza, jijini Dodoma, leo Disemba 13, 2022. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.