Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi ya Maki Brilliant Mwalimu Shaibu Beya,akizungumza na wakati wa kikao cha pamoja na Wazazi .

 Afisa Elimu wa Kata ya Buingiri David Lotto,akizungumza na wakati wa kikao  cha Wazazi pamoja na uongozi wa Shule ya Awali na Msingi ya Maki Brilliant

Diwani wa kata ya Buigiri Mhe. Keneth Yindi,akizungumza wakati wa kikao  cha Wazazi pamoja na uongozi wa Shule ya Awali na Msingi ya Maki Brilliant

WANAFUNZI wa Shule ya Awali na Msingi Maki Brilliant,wakicheza ngoma ya asili ya Kigogo wakati wa kikao cha Wazazi pamoja na uongozi wa Shule hiyo.

WANAFUNZI wa Shule ya Awali na Msingi Maki Brilliant,wakiigiza igizo la maadili  wakati wa kikao cha Wazazi pamoja na uongozi wa Shule hiyo.

…………………..

SHULE ya MAKI BRILLIANT imesema kuwa itaendelea kutoa Elimu kwa  Vitendo na kuzingatia mabadiliko ya teknolojia inayotaka ujuzi na ubunifu zaidi ili kusaidia watoto wanaosoma shuleni hapo kuwa na uwezo wa kutoa masuluhisho changamoto mbalimbali.

MAKI BRILLIANT PRE AND PRIMARY ENGLISH SCHOOL imesajiliwa  Feb 28 ,2022 ikiwa na wanafunzi tisa (9) ambapo hadi kufikia sasa wana jumla ya wanafunzi 60 kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la Sita na kwa sasa Shule ya MAKI BRILLIANT inapokea watoto kuanzia miaka Mitano (5) na kuendelea kwa darasa la kwanza (01) hadi darasa la sita (6) hivyo inatoa wito kwa Wazazi kuwaleta watoto wao kwani ni kitovu cha elimu kwa sasa katika Jiji la Dodoma.

Akizungumza wakati wa kikao cha   Wazazi  shuleni hapo Mkuu wa Shule hiyo Shaibu Beya amesema kuwa MAKI BRILLIANT imejipambanua kutoa kizazi chenye ujuzi ambacho kitakuwa na uwezo mkubwa wa kutoa masuluhisho ya changamoto.

“Mwanafunzi wa MAKI BRILLIANT ana uwezo wa kufanya jambo ambalo mwanafunzi wa chuo anakifanya kwa sababu hapa tunafundisha wanafunzi kuelewa sio kukariri ni vitendo zaidi na muda mwingine wanafunzi wetu wanasoma kwa njia ya TV tunawawekea clip zenye masomo wanasoma,”Amesema Shaibu

Moja ya sifa ya shule yetu inawalea Watoto katika maadili ya Dini na Uzalendo na imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo na ufaulu na tuna nyongeza ya kufundisha watoto Kifaransa na Kichina.

Shule MAKI BRILLIANT  inatoa Elimu ya awali,yaani Nursery School (Baby,Middle na Pre-Unit) na inapokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu (3) na shule yetu inafuata mtaala wa Wizara ya Elimu,Sayansi naTeknolojia.

Shule ya MAKI BRILLIANT  inafundisha watoto kwa vitendo hivyo watakapomaliza masomo yao wanaweza kufanya jambo lolote kwani watakuwa na maarifa na ujuzi wa kufanya kwa vitendo.

Naye Mtaalamu wa Mambo ya Elimu Ndugu Lucas Pinda ametoa wito kwa Wazazi kufanya uchaguzi sahihi pindi wanapofanya maamuzi ya kuwatafutia watoto wao shule, ikiwemo kujua historia ya wamiliki wa shule.

“Nitoe wito kwa wazazi wenzangu tunapo fanya taratibu za kutafuta shule basi tuanze kuwatambua wamiliki sio unakwenda tu kumuandikisha mtoto shule lazima ujue walau kidogo historiw yake ili usifanye maamuzi ambayo unaweza kuja kuyajutia baadae,”Amesema Pinda

Pinda amesema kuwa kwa sasa MAKI BRILLIANT ndio jibu la Wanadodoma ni shule ya uhakika yenye malengo makubwa na Mkurugenzi wake ana moyo wa kujitolea sana hivyo amewatoa wasiwasi wazazi wanaotafuta shule kwa ajili ya mwakani wafike MAKI BRILLIANT milango ipo wazi na nafasi pia zipo kwa wale wanaohitaji kuhamia darasa la kwanza mpaka darasa la Sita.

“Mkurugenzi ana upendo sana na jambo la kufurahisha ametoa nafasi 15 za bure kabisa za wanafunzi watakaotaka kuhamia Darasa la 5 na darasa la 6 hivyo kwa moyo huu tunapasawa kumuunga mkono na Wazazi jitokezeni kuchangamkia nafasi hiyo,”Ameeleza Pinda

Kwa upande wao wazazi wameushukuru uongozi wa shule kwa kuanza kujenga mabweni  yatakayo saidia watoto wao kubaki shuleni ili kuepukana na changamoto ya usafiri inayoikabili shule hiyo kwa sasa.

“Kwa niaba ya Wazazi tunawashukuru viongozi wote wa shule ya MAKI BRILLIANT  kwa hatua hii mlioichukuwa kujenga mabweni ili kuokoa adha ya usafiri inayoikabili shule yetu kwani watoto wengi wanachelewa kufika shuleni kwa kuchelewa kufuatwa na Gari”Amesema Mzazi

Vilevile wazazi wameomba ujenzi wa uzio wa shule kujengwa kwa Haraka kwani kipindi cha Mvua kinaweza kikaleta Maafa kutokana na umbali mfupi uliopo kati ya shule na korongo linalosafirisha Maji kipindi cha Masika.