Mashabiki walikuwa wakifuatilia fainali ya Kihenzile Cup and awards
**********************
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mashindano ya kihenzile cup and awards 2022 yametamatika kwa timu ya Igowole FC kuibu bigwa baada ya kuifunga timu ya Nyololo kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kufungana goli 2-2 ndani ya dakika 90 mchezo huo ulichezwa katika kiwanja cha shule ya msingi Igowole.
Kwa ushindi huo Timu ya Igowole imefanikiwa kujinyakulia kiasi Cha shilingi laki 5, Jezi seti 2, mipira miwili, Na T-shirt ambayo atavaa nahodha wa timu Hiyo.
Timu ya Nyololo iliyoambulia nafasi ya Pili imepewa kiasi Cha shillingi Laki 3, Jezi seti 2 na Mipira miwili pamoja na t-shirt Moja Kwa ajili ya Nahodha.
Kwa mujibu wa Mdhamini wa Michuano Hiyo, Mbunge wa Jimbo la Mufindi kusini David Kihenzile, Mshindi wa Tatu ambaye ni timu ya Mtwango baada ya kuifurusha timu ya Malangali Goli 7-0 amejunyakulia Shillingi Laki 1, Jezi seti 1 na T-shirt ya Nahodha.
Kihenzile alisema kuwa Lengo la michuano Hiyo ni kuibua vipaji vya vijana katika Jimbo la Mufindi Kusini na kuwaepusha na makundi hatarishi.
Alisema kuwa atawasemea wanamichezo bungeni ili serikali iweze kupunguza Kodi ya vifaa vya michezo Kwa lengo la kuwatengeneza vijana Kwa faida ya Timu za Tanzania na Taifa kwa ujumla
Kihenzile alisema kuwa katika Kutambua mchango wa shule za msingi zilizofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu, ametoa zawadi kwa shule ya tatu za halmashauri ya wilaya ya Mufindi ili kuhamasisha Taaluma.
Katika fainali ya Kihenzile Cup and awards Mgeni Rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala na Utawala Bora Deogratius Ndejembi alimpongeza Kihenzile Kwa kuanzisha mashindano Hayo huku akimtaka kuandaa Combine ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano hayo ili waweze kuunda Timu ambayo itaenda kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Combine ya Chamwino Jijini Dodoma.
Mashindano Hayo yamehusisha Timu 16 kutoka katika kata za Jimbo la Mufindi kusini yameshuhudiwa na Mwandishi Nguli wa Habari za Michezo hapa Nchini Shaffih Dauda ambaye ameahidi kuwachukua vijana waliofanya vizuri ili kuwapeleka katika vilabu vikubwa na kufanya majaribio.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Tanzania bara NEC, Mh. Richard Kasesela amewapongeza washindi waliopatikana katika michuano hiyo ya Kihenzile Cup huku akiwasisitiza vijana watakaopata nafasi ya kuchaguliwa na Mwanahabari Dauda kwenda kufanya majaribio, kuonesha nidhamu na kufanya vizuri ili kuwashawishi Maskauti wengine kuja Mkoani Iringa kutafuta wachezaji wenye vipaji vya Mpira.