Akizungumza baada ya kumtangaza mshindi, Mathipula ameipongeza Smile FM redio kwa kuandaa Mashindano hayo pamoja na Kampuni ya Mati super Brand Ltd kwa kudhamini shindano huku akikumbusha wadau wengine kusaidia washiriki wa shindano hilo ili wasipotee kama ambavyo washiriki wa Mashindano kama hayo wanavyopotea.
“Washiriki wote ni washindi na wana vipaji vikubwa, Smile fm na Mati Super Brand naomba muwachukue vijana hawa muwasaidie ili wasipotee” Amesema.
Mkurugenzi wa Smile fm redio Jamal Mteri, amesema washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye Kumi Bora wataunda Band Moja na kukabidhiwa vifaa vitakavyosaidia kufanya kazi kwa Pamoja.
Milka amejinyakulia Shilingi Laki 5 kutokana kwa mdhamini MATI SUPER BRAND kupitia Kinywaji Cha Strong Dry Gin.
Akizungumza na Smile fm Milka ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili, amesema wakati anaingia kwenye shindano hilo hakutegemea kama angeshinda kutokana na ushindani uliokuwepo kutoka kwa washiriki wengine.
Aidha, wakati Milka akishehereka ushindi namba moja, nyuma yake alikuwepo mshiriki Chief Kiara kutoka Nakwa aliyeshinda nafasi ya pili akipewa shilingi Laki mbili na nusu na nafasi ya tatu ilikamatwa na Abby Nation akichukua Shilingi Laki Moja na nusu.
Kabla ya Milka kutangazwa mshindi hakuonesha dalili za waziwazi kwani watatu hao walikuwa wanachuana vikali.
Kila aliyepanda jukwaani alipagawisha watu na kusababisha shangwe Kubwa kutoka kwa mamia ya watu waliofurika Uwanjani hapo.
Waigizaji walikuwa wawili, Sadam na Haji ambapo Sadam alitolewa hatua ya nusu fainali huku Haji akifanikiwa kufika fainali na kushia Tano Bora.