Hatimaye Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia zimefikia tamati leo jijini Tanga kwa kutanguliwa na maandamano yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wengine waliopo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.
Akizungumza katika kilele hicho Katika Viwanja vya Tangamano Mkuu wa Wilaya ya Tanga HASHIM MGANDILWA amewataka Wananchi na wazazi kwa ujumla kupunguza ukarimu kwa wageni ambao wamekuwa wakiwalaza na Watoto wao jambo ambalo limekuwa ni kichocheo kimojawapo cha kushamiri vitendo vya ukatili hususani kwa Watoto.
FOOTAGE: HASHIM MGANDILWA – MKUU WA WILAYA TANGA
Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi ACP Faidha Suleiman amewataka wadau kuendelea kuunganisha nguvu katika mapambano hayo.
FOOTAGE 2: ACP Faidha Suleima- Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Polisi Makao Makuu
VOX POP
- Sikudhani Shabani- Shirika la LSF
- SACP Henry Mwaibambe- Kamanda wa Polisi Mkoa waTanga
Jeshi la Polisi limekuwa likiadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili kila mwaka ambapo limekuwa likitumia siku hizo kuunganisha nguvu katika kutoa elimu ambapo mwaka huu Watendaji wote wa Madawati kutoka Tanzania bara na Zanzibar walitoa elimu katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.