Mwaklishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshmiwa Pololet Mgema akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na wiki ya watoa msaada wa kisheria kimkoa iliyofanyika katika viwanja vya Black Belt Kata ya Ruvuma Manispaa ya Sopngea
Afisa Maendeleo ya Jamii katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira akitoa ya ukatili wa kijinsia na watoto katika maadhimisho ya siku 16 za kuoinga ukatili wa kijinsi Mkoa wa Ruvuma kwenye viwanja vya Black belt Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea
BAADHI ya wananchi wakiwemo wanawake na watoto wa Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema
NGOMA maarufu ya lizombe ya kikundi cha Shamba kutoka mjini Songea ikitumbuiza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kuoinga ukatili wa kijinsia katika Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea
………………………….
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hali ya vitendo vya ukatili katika Mkoa ni mbaya hivyo jamii yote inatakiwa kuwajibika ili kuhakikisha ukatili unakoma.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema, katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili na wiki ya watoa msaada wa kisheria katika hafla iliyofanyika kimkoa katika viwanja wa Black Belt Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea,RC Thomas ameyataja matukio yaliyoripotiwa katika Jeshi la Polisi kwa kipindi cha miezi sita iliyopita mkoani Ruvuma yalikuwa 442.
Ameyataja baadhi ya matukio hayo kuwa ni kubaka matukio 24,shambulio la aibu matukio 45,mimba kwa wanafunzi matukio 49,shambulio la kudhuru mwali matukio 86 na kutumia lugha za matusi matukio 42.
“Katika jamii zetu ukatili umeshika kasi kubwa sana katika kipindi hiki,madhara ambayo yanasababishwa na vitendo vya ukatili ni kama vile kupoteza Maisha,ulemavu wa kudumu,msongo wa mawazo,umasikini mkubwa unaotokana na kushindwa kuwajibika na kuongezeka kwa Watoto wa mitaani’’,alisema RC Thomas.
Akizungumzia wiki ya watoa msaada wa kisheria katika Mkoa wa Ruvuma,RC Thomas amewataja moja ya kazi za Watoa Msaada wa Kisheria kuwa ni kusaidia mtu anapokutwa na hatari ya kufanyiwa ukatili na uonevu mwingine wowote.
Hata hivyo ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu na kujenga jamii huru katika shughuli za ujenzi wa Taifa.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Jeshi la Polisi nchini,katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba 2021,mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili ni Arusha,Tanga,Shinyanga,Mwanza na Mkoa wa kipolisi wa Ilala (Dar es salaam).
Akitoa taarifa ya ukatili wa kijinsia na watoto kwenye maadhimisho hayo,Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira amezitaja aina tatu za ukatili kuwa ni ukatili wa kimwili ikiwemo vipigo na kujeruwi.
Mlimira ameitaja aina nyingine kuwa ni ukatili wa kingono ikiwemo ubakaji na ulawiti,ukatili wa kisaikolojia ikiwemo matusi na kejeli,ukatili wa kiuchumi ikiwemo kutelekeza familia na ukatili wa unyonyaji ikiwemo kutumikisha kwa kulipa ujira mdogo.
Hata hivyo amezitaja shughuli zilizofanyika katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili,mkoani Ruvuma kuwa ni kutoa elimu ya ukatili,kufanya mikutano katika Taasisi za kidini,kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na Kwenda kuwatembelea Watoto yatima.
Naye Mshauri Mkuu wa Masuala ya kijinsia na Mwakilishi wa Mradi wa Afya Yangu katika Mkoa wa Ruvuma John Toto amesema katika juhudi za kupambana na ukatili wa kijinsia mradi huo kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wameendesha mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma za afya 88 waliopata mafunzo ya kusaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2022 ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni Kila uhai una thamani: Tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.
Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma