Wahitimu wa mafunzo ya Usaidizi wa Maabara wakiandamana wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale Kulwa akikabidhi keki kwa wahitimu
Na Mwandishi wetu – Malunde 1 blog
Mahafali ya Kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
kilichopo mtaa wa Magobeko kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Desemba 9,2022 ambapo jumla ya Wanafunzi 20 wamehitimu mafunzo ya Usaidizi wa Maabara kati yao wavulana ni 7 na wasichana 13.
Akitoa taarifa ya mafunzo katika chuo hicho ,mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Mwalimu wa taaluma wa Chuo cha Hill Forest College Shinyanga John Mtaka amesema kuwa chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 150 na kinatoa mafunzo katika fani tatu ambazo ni fani ya Wasaidizi wa maabara ,Utalii na Mapishi pamoja na kozi ya Computer.
Pia Mtaka amebainisha kuwa chuo kimefanya vizuri katika matokeo yake ambapo wahitimu wamefanikiwa kufanya vizuri katika mitihani yao na kufanikiwa kushika nafasi ya 1,2,3 na ya 4 katika vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi Veta ngazi ya cheti katika kozi ya Wasaidizi wa maabara nchini.
Mkuu wa Chuo cha Hill Forest College Shinyanga David Kanuda ameeleza kuwa wameweka mkakati wa kuboresha mazingira ya chuo ikiwemo kuongeza mabweni ya chuo kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho wakitokea nje ya mkoa wa Shinyanga.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye ni diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale Kulwa ameupongeza uongozi wa chuo hicho pamoja na wanafunzi kwa kufanya vizuri katika mitihani yao na kuitangaza kata ya Ibadakuli na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla huku akieleza kuwa changamoto zilizo elezwa na uongozi wa chuo ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa maji na umeme ataitafutia ufumbuzi kwa kuifikisha katika vikao vya maendeleo ya kata na taasisi zinazohusika na utatuzi wa changamoto hiyo.
Pia Msabila amewaasa wazazi na walezi wakata hiyo kuwapeleka watoto wao katika chuo hicho ili waweze kupata elimu bora itakayo wasaidia wao kujiajiri na kumudu katika soko la ushindani .
Wahitimu wa mafunzo ya Usaidizi wa Maabara katika Chuo cha Hill Forest College Shinyanga wakiandamana wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga leo Ijumaa Desemba 9,2022 – Picha na Mpiga Picha wa Malunde 1 blog
Wahitimu wa mafunzo ya Usaidizi wa Maabara wakiandamana wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mgeni rasmi Mhe. Msabila Malale na viongozi mbalimbali wakielekea ukumbini wakati Wahitimu wa mafunzo ya Usaidizi wa Maabara wakiandamana kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale Kulwa akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale Kulwa akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mkuu wa Chuo cha Hill Forest College Shinyanga David Kanuda akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Mwalimu wa taaluma John Mtaka akitoa taarifa ya mafunzo kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Daniel Emmanuel Manga akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mhitimu, Edina Peter Makolo akisoma risala kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Wahitimu wa Mafunzo ya Usaidizi wa Maabara wakionesha kwa vitendo namna wanavyofanya kazi wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Wahitimu wa Mafunzo ya Usaidizi wa Maabara wakionesha kwa vitendo namna wanavyofanya kazi wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo cha Hill Forest College Shinyanga
Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale Kulwa akikabidhi keki kwa wahitimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Hill Forest College, Daniel Emmanuel Manga na Mkuu wa Chuo cha Hill Forest College Shinyanga David Kanuda wakikabidhi keki kwa wazazi (kushoto)
Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale Kulwa akikabidhi keki kwa Mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Mwalimu wa taaluma John Mtaka
Burudani ikiendelea
Washiriki Onesho la Fashion wakipiga picha ya kumbukumbu
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali