Baadhi ya Watendaji wa Dawati hilo wakitoa elimu.
……………………
Na. A/INSP FRANK LUKWARO- TANGA
Watendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar wapo Mkoani Tanga kwa ajili ya kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia pamoja na kuifanya Mkutano wa mwaka wa Dawati hilo ambapo katika maadhimisho hayo wameendelea na Zoezi la kutoa elimu ya kuepukana na vitendo vya Ukatili katika Maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Maeneo yaliyofikiwa ni pamoja na Shule za Msingi na Sekondari, Vijiwe, Masoko na kwenye mikusanyiko yenye watu wengi ambapo kwa pamoja Watendaji hao wametoa elimu kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali za Mitaa na Kata pamoja na Maafisa Ustawi Jamii.
Utaratibu huo wa kutoa Elimu umelenga kufikia pia baadhi ya Wilaya za mkoa huo hususani katika maeneo ya Barabara kuu ambayo yana mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuwafikia watu wengi zaidi.