Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, James Ruge alisema jana wakati akitoa kwa waandihi wa habari taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa robo ya kwanza kuanzia Julai hadi Septemba 2022.
Amesema katika robo ya pili ya Oktoba hadi Disemba 2022, TAKUKURU mkoani Mwanza itendelea kutekeleza ajuumu yake kkwa mujibu wa sheria.
Ruge amesema katika kuzuia rushwa kwenye miradi ya maendeleo itakagua na kusimamia kwa karibu matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali kutekeleza mirdi hiyo ili thamani ya fedha hizo ionekane.
Amesema mkakati wa pili ni kuchunguza makosa kwa wot watakaojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
“Elimu yaa mapambano dhidi ya rushwa itatolewa zaidi kupitia vyombo vya habari (redio,magazeti, luning na mitandao ya kijamii) na utaratibu wa TAKUKURU inayotembea katika kuhakikisha inawafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao na kuwaelimisha umuhimu na wajibu wao kusimamia miradi ya maendeleo ,”amesema Ruge.
Amesema anaamini njia hiyo itaongeza na kupanua wigo wa ushirikishaji wananchi katika kuzuia na kupambana na rushwa kama ilivyo kauli mbiu ya mapambano dhidi ya rushwa ‘Kuzuia Rushwa ni Jukumu langu na lako; Tutimize Wajibu Wetu.’