Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Hamis akikabidhi vyeti kwa wahimu waliofanya vizuri kitaaluma katika Mahafali ya 46 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Hamis akizungumza katika Mahafali ya 46 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni akizungumza katika Mahafali ya 46 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju akiwa katika Mahafali ya 46 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Wahitimu wakiwa kwenye maandamano katika Mahafali ya 46 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KATIKA mwaka wa fedha 2022/23, Taasisi ya Ustawi wa Jamii imepanga kuanza ujenzi wa hosteli zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 na ukumbi wa mihadhara wenye kuchukua wanafunzi 380 katika kampasi ya Dar es Salaam.
Ameyasema hayo leo Desemba 8,2022 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii , Dkt. Fidelis Mafumiko katika Mahafali ya 46 ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Amesema kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita, Taasisi imeendelea kujiimarisha katika kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa huduma kwa jamii.
Aidha amesema Taasisi imefanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 2,542 (Ke 1,680 na Me 862) waliodahiliwa mwaka 2020/21 hadi kudahili wanafunzi 3,234 (Ke 2,104 na Me 1,130) mwaka 2021/22.Hili ni ongezeko la asilimia 27.2%.
Amesema Taasisi inatoa wahitimu mahiri na huduma bora kwa Jamii, Bodi ya Magavana imekuwa ikisisitiza watumishi kujiendeleza ili kuimarisha ujuzi wao.
“Hivyo, kwa sasa watumishi 44 wako katika mafunzo ya muda mrefu ambapo jumla ya watumishi 31 wanasoma Shahada ya Uzamivu, 08 Shahada ya Uzamili, 03 Shahada ya kwanza na 02 Diploma. Miongoni mwao wanataaluma ni 33 na 11 waendeshaji”. Amesema
Nae Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni amesema katika fani ya Ustawi wa Jamii, jumla ya wahitimu 1,246 wamefaulu. Miongoni mwao, wahitimu 937 sawa na asilimia 75 ni wanawake na wahitimu 309 sawa na asilimia 25 ni wanaume.
Hata hivyo amesema katika fani ya Menejimenti ya Rasilimali Watu, jumla ya wahitimu 977 wamefaulu. Kati ya hao, wahitimu 731 sawa na asilimia 75 ni wanawake na wahitimu 246 sawa na asilimia 25 ni wanaume.
“Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kutuamini kama Taasisi ambayo imebobea katika kutoa Elimu ya umahiri kwa kuendelea kutuletea wanafunzi kupitia TAMISEMI kwani kwa miaka mitatu mfululizo imetuletea wanafunzi wengi katika ngazi ya Astashahada (cheti)”. Amesema