*******************
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Lawrence Mafuru amewataka Wanamipango kusaidia nchi kupanga na kuweka mikakati ya mipango mbalimbali ya Maendeleo inayolenga kuiwezesha nchi kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi.
Bw. Mafuru alisema hayo wakati wa kufunga kongamanola mwaka la wanamipango lililofanyika Jijini Dar es Salaam.
Bw. Mafuru alisema Wanamipango katika Taifa lolote lile Ulimwenguni ndio huamua Taifa liweje, hivyo aliwataka kuhakikisha Mipango wanayopanga inakuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho ili kuweza kuitendea haki kada ya Wanamipango nchini.
‘Dhima ya mwaka huu la kongamano hili inaonesha umuhimu wa kada ya wanamipango kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kizazi kijacho na pia inatukumbusha kuwa wanamipango katika Taifa lolote lile ulimwenguni ndio huamua Taifa liweje, hivyo mnawajibu wa kuhakikisha Mipango mnayoipanga ina manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho na kwa kufanya hivyo tutakuwa tukiitendea haki kada hii na Taifa litawakumbuka’ . Alisema Bw. Mafuru
Bw. Mafuru amewataka wanamipango kuhakikisha masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwa muda wa siku tatu za Kongamano hilo na maazimio yaliyofikiwa yatumike kikamilifu katika maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kutokana na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kukaribia mwisho.
Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango itahakikisha maandalizi ya Dira mpya ya Maendeleo 2050 yanakuwashirikishi ili kupata Dira itakayosaidia kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi kwa haraka.
Aidha, Bw. Mafuru aliwashukuru washiriki wa kongamano hilo kwa kujadili kwa weledi mkubwa masuala mbalimbali yakiwemo ya umasikini, mipango ya maendeleo na uhimilivu wa deni la Serikali, elimu, maarifa na ujuzi kwa ajili ya kuchochea ushindani, kuajiri na ubunifu na mienendo na mabadiliko ya idadi ya watu na athari zake katika maendeleo ya Tanzania kwa siku zijazo.
Bw. Mafuru aliwataka Washiriki wa kongamano hilokutambua hatma bora kwa Taifa kwa miaka 25 ijayo kuwa ipo mikononi mwa Wanamipango na kuwataka kuwa mabalozi kwa Wananchi pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Sekretarieti na timu ya uandishi pindi watakapo anza zoezi la kupata Maoni na ushauri kwenyemaandalizi ya Dira mpya ya Maendeleo ya 2050.
Bw. Mafuru aliwahakikishia washiriki wa kongamano hilona Wananchi kwa ujumla kuwa Maoni na ushauri utakaotolewa, Serikali utaufanyia kazi ili kuwezesha Mipango yetu inatumika ili kuiletea nchi maendeleo.
Kwa upande wake Kamishina wa Idara ya Mipango ya Kitaifa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi alisema kongamano hilo la siku tatu hufanyika kila mwaka kwa lengo la kubadilishana mawazo na uzoefu ili ujuzi unaopatikana kutoka kwa washiriki utumike katika kuboresha ufanisi wa kazi katika maeneo mbalimbali nchini.
Dkt. Milanzi alisema kuwa kongamano hilo limekuwa na manufaa makubwa kwa Wanamipango kutokana na umuhimu wao katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi unaotokana na kupanga, kusimamia, na kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
‘Ni dhahiri uwepo wetu hapa kwa siku tatu umekuwa wa manufaa makubwa kwetu. Tumepata wasaa wa kujadili, kutafakari na kubadilishana mawazo, maarifa, uzoefu nahata kuongeza idadi ya marafiki. Hivyo, ni rai yangu tutumie ujuzi tulioupata hapa katika kuboresha ufanisi wa kazi katika maeneo yetu’.Alisema Dkt. Milanzi
Akizungumza katika kongamano hilo Kamishina Msaidiziwa Idara ya Mipango ya Kitaifa , Bw. Royal Lyanga alisema ili kuboresha utendaji kazi wa wanamipango nchini, Wizara ya Fedha na Mipango imefanyia kazi maoni ya wadau mbalimbali kwa kuanzisha kanzidata ya wanamipango itakayosaidia kufuatilia taarifa mbalimbali za ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali nchini.
Bw. Lyanga aliongeza kuwa ili kuleta ufanisi katika utendaji wa kanzidata hiyo amewaomba wanamipango wote nchini kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi pindi taarifa hizo zitakapohitajika.
Kongamano la wanamipango hufanyika kila mwaka ambalo huwakutanisha wanamipango,