Mwenyekiti wa mafunzo ya elimu ya kazi kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya,Emmanuel Mwangomo akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Mkuu wa chuo cha wafanyakazi Tanzania kilichopo Mbeya ,Hezron Kaaya akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha .
**********************
Julieth Laizer Arusha .
Arusha.Imeelezwa kuwa,kuwepo kwa elimu ya kutosha juu ya mafunzo ya kazi mahala pa kazi yanaongeza kwa kiasi kikubwa mahusiano mazuri kazini pamoja ufanisi na utendaji kazi.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkuu wa chuo cha wafanyakazi Tanzania kilichopo mkoani Mbeya , Hezron Kaaya wakati akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa menejiment na viongozi wa tawi la wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali za kazi nchini.
Kaaya amesema kuwa ,lengo la mafunzo hayo ni kuangalia namna ya kujenga mahusiano bora na menejiment na chama cha wafanyakazi na kuweza kuongeza tija mahala pa kazi na kuongeza uzalishaji
Amesema kuwa ,utafiti unaonyesha kuwa sehemu za kazi ambapo viongozi walipita na kupatiwa mafunzo ya vyuo na Ufanisi wa kazi unakuwa mkubwa zaidi.
“unajua kunapokuwepo na mafunzo ya kazi mara kwa mara yanasaidia sana utendaji kazi kuboreka na kufanyika kwa ufanisi mkubwa huku uzalishaji ukiongezeka zaidi mahala pa kazi kutokana na kuwepo kwa mahusiano mazuri kazini. “amesema Kaaya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mafunzo ya elimu ya kazi kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya,Emmanuel Mwangomo amesema kuwa ,mafunzo hayo ya kazi yanawapa faida kubwa sana kwani yanawajengea mahusiano katika ngazi ya wafanyakazi na waajiri wao pamoja na viongozi wa wafanyakazi na waajiri wao.
Mwangomo amesema kuwa ,sio kila kiongozi amesomea maswala ya elimu kazi ni viongozi wachache sana wenye elimu hiyo ambayo inasaidia kujua jinsi ya kutetea maslahi ya wafanyakazi pamoja na kutengeza mahusiano mazuri ya wadau wa kazi.
“Ni jambo la muhimu sana viongozi kuhakikisha wanapata elimu hiyo kwani ni lazima kuwepo kwa mahusiano mazuri sehemu za kazi ili kuongeza mshikamano na tija katika sehemu za kazi.”amesema .
Aidha washiriki zaidi ya 50 wameweza kushiriki mafunzo hayo ambayo yataongeza mshikamano na tija kwenye sehemu za kazi huku mada kuu katika semina hiyo ni namna ya kujenga mahusiano bora baina ya menejiment na chama cha wafanyakazi kwa ajili ya kuongeza tija na kuleta ustawi mzuri wa wafanyakazi.