WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu wenye lengo la kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa elimu kushiriki kikamilifu katika kupanga Mipango ya Maendeleo ya Elimu na Programu kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu kwa mtu mmoja mmoja, jamii na taifa kwa ujumla unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.
SEHEMU ya Wadau wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu pamoja na wanafunzi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu Tanzania Bi.Faith Shayo,akitoa maoni wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.
Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bw.Ocholo Wayoga,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.
……………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ,amesema Mwamko wa kufanya mageuzi ya elimu ni ajenda iliyopo Duniani kote na kwamba Tanzania imewahi kuanza mageuzi hayo.
Hayo ameyasema leo Disemba 6,2022 jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa mwaka wa kufanya mapitio ya Sekta ya elimu ambapo amewaomba wadau hao kushiriki katika mageuzi hayo.
Prof.Mkenda amewapongeza wadau kwa namna wanavyoshiriki kikamilifu kutoa maoni yao madhubuti kwa ajili ya kusaidia Mageuzi Makubwa katika sekta ya Elimu nchini.
”Sekata ya Elimu nchini bado inahitaji mageuzi makubwa hivyo anaamini kupitia mkutano huo Wadau watapata nafasi ya kujadi kikamilifu namna ya kuleta maendeleo endelevu kwenye sekta ya Elimu.
“Baada ya Rais Samia kuingia madarakani alitoa maelekezo ya kufanya mapitio ya Sera na mabadiliko ya mitaala kwa lengo la kuhakikisha elimu inayotolewa inaendelea kuwa bora na kutoa elimu ujuzi. Niwaombe wadau tuendelee kushirikiana katika kuboresha na kukuza elimu nchini,” amesema Prof Mkenda.
Aidha Waziri Mkenda amewataka wadau hao kuwa mapitio ya sera na mitaala yameshirikisha wadau mbalimbali na kwamba kwa sasa yapo tayari kwa mjadala wa kitaifa kuhusu mapendekezo ya sera ya elimu na mitaala.