Mkurugenzi wa Biashara Halotel, Bw; Abdallah Salum, akizungumza na waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu (Chuo) nchi nzima ambapo Kampuni ya Simu ya Halotel itakuwa inampatia kila mwananfunzi wa elimu ya Juu anayetumia laini ya mwanachuo iitwayo (EDU SIMs) ya Halotel salio la bure lenye thamani ya shilingi 1500 kila mwezi litakalomwezesha kutumia katika kujiunga na kifurushi cha intaneti na kuwasaidia kwenye masomo yao. Pamoja naye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko Sakina Makabu (kulia) Na Afisa Masoko HaloPesa Roxana Kadio (Kulia).
Mkuu wa Kitengo cha masoko Halotel Sakina Makabu, akizungumza na waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu (Chuo) nchi nzima ambapo Kampuni ya Simu ya Halotel itakuwa inampatia kila mwananfunzi wa elimu ya Juu anayetumia laini ya mwanachuo iitwayo (EDU SIMs) ya Halotel salio la bure lenye thamani ya shilingi 1500 kila mwezi sambamba na hili Kila mwanachuo anayetumia laini ya Halotel ya mwanachuo ataweza kutumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia HaloPesa bila tozo za serikali. Huduma hii itaendeshwa kwa miezi sita kuanzia Desemba 2022, na wanafunzi wenye laini hizo wataweza kufanya miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000.
Afisa Masoko wa HaloPesa Roxana Kadio akiongea na waandishi wa Habari leo katika uzinduzi wa wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu (Chuo) nchi nzima ambapo Kampuni ya Simu ya Halotel itakuwa inampatia kila mwananfunzi wa elimu ya Juu anayetumia laini ya mwanachuo iitwayo (EDU SIMs) ya Halotel salio la bure lenye thamani ya shilingi 1500 kila mwezi sambamba na hili Kila mwanachuo anayetumia laini ya Halotel ya mwanachuo ataweza kutumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia HaloPesa bila tozo za serikali. Huduma hii itaendeshwa kwa miezi sita kuanzia Desemba 2022, na wanafunzi wenye laini hizo wataweza kufanya miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000. Pamoja naye ni Mkurugenzi wa Biashara Halotel Bwa Abdallah Salum (kushoto) Na Mkuu wa Kitengo cha Masoko sakina Makabu (Kulia)
Rais wa Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Bw; Spencer Minja, akiipongeza kampuni ya simu Halotel mbele ya waandishi wa habari, kwa ubunifu huo wa kuja na huduma ambayo utawasaidia wanafunzi kusoma kidijitali kwa kujiunga na vifurushi vya intaneti kupitia salo hilo la bure kila mwezi katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu (Chuo) nchi nzima ambapo Kampuni ya Simu ya Halotel itakuwa inampatia kila mwananfunzi wa elimu ya Juu anayetumia laini ya mwanachuo ya Halotel salio lenye thamani ya shilingi 1500 kila mwezi, kuanzia wanapojiunga chuo mpaka wanapomaliza. Pamoja naye ni Rais wa Uongozi wa Chuo Cha NIT Dar es salaamu.
Shughuli za Usajili wa Laini za Mwananchuo zikiendelea katika eneo la Chuo kikuu cha Dar es Salaam Leo wakati wa uzinduzi wa Huduma mpya kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu (Chuo) nchi nzima ambapo Kampuni ya Simu ya Halotel itakuwa inampatia kila mwanafunzi wa elimu ya Juu anayetumia laini ya mwanachuo ya Halotel salio lenye thamani ya shilingi 1500 kila mwezi sambamba na hili Kila mwanachuo anayetumia laini ya Halotel ya mwanachuo ataweza huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia HaloPesa bila tozo za serikali. Huduma hii itaedeshwa kwa miezi sita kuanzia Desemba 2022, na wanafunzi wenye laini hizo wataweza kufanya miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000.
***********************
DAR ES SALAAM 06 Desemba 2022……… Katika juhudi zake za kusaidia sekta ya elimu hapa nchini, Kampuni ya Halotel imekuja na ubunifu mwingine katika kutoa huduma zake kwa wateja.
Leo kampuni imetangaza huduma mpya inayolenga kuchochea usomaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu kupitia mitandao ambapo kampuni itakuwa inampatia kila mwanafunzi anayetumia laini ya Mwanachuo ya Halotel salio lenye thamani ya shilingi 1500 kila mwezi.
Huduma hii mpya inategemewa kuboresha kujifunza kupitia mtandao miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini.
“Tungependa kuwa sehemu ya maendeleo ya sekta hii muhimu. Tunaelewa kuwa elimu huwezesha watu kuendeleza vipaji vyao na kuwa watu wenye mafanikio katika jamii. Amesema Mkurugenzi wa Biashara Halotel Bw. Abdallah Salum.
“Kwa kuchangia sekta hii kupitia mradi wa maendeleo ya kijamii, tunaamini kuwa tutasaidia kupunguza hali ya kutokuwepo kwa usawa na hivyo kufanya maendeleo jumuishi ya rasimali watu kwa kuwawezesha wanafunzi kupata na kufurahi fursa wezeshi na zenye tija kidigitali katika masomo na maisha kwa ujumla,” amesema Bwa; Abdallah Salum.
Mkurugenzi huyo wa Biashara amesema kuwa huduma hiyo ni endelevu kwa vile kampuni inalenga kukuza na kusaidia wanafunzi wote wa elimu ya juu kwa kuwapa salio lenye thamani ya shilingi 1500 kuanzia wanapoanza masomo chuoni hadi watakapomaliza.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2022 kutoka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa makadirio kwa sasa kuna jumla ya wanafunzi wapatao 900,000 katika taasisi za elimu ya juu hapa nchini.
Jumla ya vyuo vikuu vipatavyo 280 na zaidi vimejumuishwa katika programu hii ya Halotel.
Pamoja na kuzindua na kutoa huduma hii, kampuni imepanga kuandaa tamasha kubwa mnamo tarehe 10 mwezi Desemba mwaka huu.
Tamasha hili litajumuisha burudani kutoka kwa wasanii maarufu ikiwemo Mr Blue, Mabantu, Sarafina, Dullah Makabila na wengineo.
“Kuhakikisha kuwa wanafunzi wa vyuo wanafaidi huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia Halopesa, Halotel kupitia HaloPesa inaanzisha kampeni ya kutuma na kupokea pesa bila tozo za serikali kwa wateja wake amabo ni wanafunzi wa vyuo vikuu. Huduma hii itapatikana kupitia laini za mwananchuo za Halotel maalumu kwa wanafunzi ziitwazo ‘Edu SIMs’,” amesema Afisa Masoko wa Halopesa Roxana Kadio.
Kampeni hii itaendeshwa kwa miezi sita kuanzia mwezi huu wa Desemba, ambapo wanafunzi wa vyuo wanaotumia huduma ya HaloPesa wataweza kufanya miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000. Kila mwanafunzi wa chuo atakayekuwa mteja wa HaloPesa ataweza kupata Promosheni hii kwa kufanya miamala yoyote ya Halopesa.
Promosheni hii ya ‘bila tozo za serikali’ inalenga kuhamasisha zaidi matumizi ya huduma ya HaloPesa kwa wanafunzi wa vyuo na hivyo kupanua huduma za kifedha kidijitali hapa nchini.
“Tunatambua juhudi za Serikali katika kuboresha huduma ya elimu kupitia miradi mbalimbali na sera kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,” Ameongeza Roxana Kadio
Katika hotuba yake, rais wa wanafunzi…AU…Makamu Mkuu wa Chuo ameipongeza kampuni ya Halotel kwa ubunifu huo wa kuja na huduma ambayo itawasaidia wanafunzi kusoma kidijitali kwa kujiunga na vifurushi vya intaneti na hivyo kuperuzi.
Alisema kuwa kupata salio la bure la shilingi 1500 itakuwa ni msaada mkubwa kwa wanafunzi ambao wengi wana kipato kidogo.
Hivi karibuni Speedtest Global Index ilitoa ripoti yake na kuonesha kuwa kampuni ya Halotel imeongoza kampuni zingine za simu kwa kuwa na mtandao wenye kasi Zaidi ukilinganisha kampuni zote katika kipindi cha robo tatu zote kwa mwaka huu zilizoishia mwezi Septemba.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa kwa mwezi Septemba Halotel imeongoza kwa kuwa na intaneti yenye kasi ya 17.63 Mbps, ikifuatiwa na Vodacom (13.63Mbps), na Airtel (11.61Mbps).