Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Equiplus Ltd ,James Genga akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha .
**************************
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Wadau mbalimbali wameshauriwa kutumia bidhaa za kampuni ya Equiplus inayojihusisha na usambazaji wa vifaa vya maji ikiwemo pump za maji kwani vina ubora wa hali ya juu na vinadumu muda mrefu.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, James Genga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma hizo wanazotoa .
James amesema kuwa,vijana wa kitanzania asilimia 100 wamejikita kusaidia sekta ya maji kwa kusambaza pump za maji na kuzifunga katika mikoa mbalimbali nchini.
Amesema kuwa,kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2018 ambapo wamekuwa na mafanikio makubwa kwani wamekuwa wakifanya kazi na wizara ya maji na mamlaka za maji na hiyo ni kutokana na huduma nzuri wanayotoa kwa wateja wake.
“sisi bidhaa zetu tumekuwa tukitoa kwa gharama ambayo mtu yoyote anaweza kumudu na unafikishiwa mzigo ndani ya muda mfupi na kuweza kutatua changamoto za wateja wetu kwa wakati”amesema James.
Ameongeza kuwa, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kushiriki katika miradi mikubwa na midogo na kwa bei nafuu na wamekuwa wakishirikiana na wadau pamoja na makampuni binafsi , na serikali .
Aidha amewataka wadau mbalimbali kutumia kampuni hiyo kwa kuagiza bidhaa mbalimbali ambazo wataletewa kwa wakati katika maeneo yao na kuweza kupatiwa huduma inayohitajika.