****************
Na. WAF – Arusha
Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo Sightsavers inawezesha upatikanaji wa huduma za watu wenye ulemavu ikiwemo huduma za Afya, Elimu, Miundombinu pamoja na uwezeshwaji wa Kiuchumi.
Hayo ameyasema na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali (Sightsavers) Bw. Godwin Kabalika kwenye kilele cha Maadhimisho ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambapo Kitaifa yalifanyika Jijini Arusha.
“Shirika letu linashirikiana kwa Karibu na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara ya Afya kwa kuhakikisha huduma za watu wenye ulemavu pamoja na kuwapatia vifaa wezeshi ili kurahisisha shughuli zao.” Amesema Bw. Kabalika
Kwa Tanzania Shirika la Sightsavers linafanya kazi ndani ya Mikoa Mitano ambayo ni pamoja na Singida, Morogoro, Manyara, Ruvuma pamoja na Lindi kwa kushirikiana na Serikali katika eneo la vifaa, miundombinu, na utoaji wa Elimu.
Pia, Bw. Kabalika amesema miongoni mwa kazi zao wanazofanya ni pamoja na kuwajengea uwezo waajiri pamoja na walemavu ili waweze kupata ajira katika soko la ajira na hata ujasiriamali kwa kuwawesha upatikanaji wa vifaa na elimu ili waweze kudumu katika biashara hizo.
Kilele hicho cha Maadhimisho ya watu wenye ulemavu hufanyika kila mwaka tarehe 3, Desemba ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ilikua “Suluhisho Mabadiliko kwa ajili ya Maendeleo Jumuishi: Nafasi ya Ubunifu katika Kuchagiza Duniani Inayofikika na Yenye Usawa.”