Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC)William Erio wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
………………………..
Julieth Laizer ,Arusha
Waziri wa Uwekezaji,Biashara na Viwanda,Dk,Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la wadau wa mazingira na utalii litakalofanyika Jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya siku ya ushindani Duniani itakayofanyika Desemba ,5 mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC)William Erio wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Amesema kuwa, watu 120 watahudhuria kongamano hilo kwa lengo la kutunza mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwani athari za kiikolojia zinaweza kudhibitiwa ili kuhakikisha kila mtu ananufaika na mazingira rafiki kwa binadamu na wanyama.
Amesema kuwa,kauli mbiu ya kongamano hilo ni “sera ya ushindani na mabadiliko ya tabia nchi ambayo ni ya kidunia katika maadhimisho ya FCC na kwa upande wa Tanzania kauli mbiu ni ushindani na utalii endelevu”.
Erio amesema kuwa,kuongezeka kwa hewa ukaa kunachangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi yanayoleta athari katika ikolojia ikiwemo kudhibiti barafu ya Mlima Kilimanjaro kutoyeyuka ili kuongeza idadi ya watalii kuja nchini.
Amesema kuwa,mabadiliko ya mazingira yanaweza kuleta ukame hivyo lazima theluji iliyopo Mlima Kilimanjaro iendelee kuwepo kwa kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
“Lazima tulinde mazingira na wale wanaofanya shughuli za utalii walinde mazingira ili kulinda theluji ya mlima Kilimanjaro kwani ndio inayoleta watalii wengi nchini na utalii kanda ya kaskazini umeshamiri sana” Erio.
Amesema kuwa ,viongozi wengine watakaokuwepo ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango,Mwigulu Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana na mawaziri wengine au wawakilishi wao na kuongeza kuwa FCC wamefungua ofisi Mkoani Arusha kwa lengo la kutoa huduma karibu na wananchi na ofisi hizo zipo eneo la Carmatec Njiro.