Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Leonard Masanja akiongea wakati wa kikako kazi juu ya kupunguza udumavu mkoa wa Iringa kupitia Mradi wa USAID Lishe Endelevu
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa makini kuwasikiliza viongozi
Nengilangen’t
Kivuyo-Meneja Mradi wa USAID Lishe Endelevu Mkoa wa Iringa akiwa kwenye
moja la shamba la mfano.
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
MRADI wa
USAID Lishe Endelevu umeanzisha mashamba ya mfano 186 na kuwafikia na
kuwajengea uwezo wakulima 6,842 ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuusaidia
Mkoa wa Iringa kukabiliana na udumavu.
Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha katika kila watoto 100 wenye
miaka chini ya mitano mkoani humo, 47 sawa na asilimia 47 wamedumaa kutokana na
lishe duni.
Mratibu wa
USAID Lishe Endelevu (Kilimo Mifugo na Uvuvi), Samwel Kitila alisema hatua hiyo
imelenga kuiwezesha jamii kuongeza uzalishaji na ulaji wa vyakula vyenye
virutubishi vingi.
Aliongeza kwa kusema kuwa Mradi wa USAID Lishe Endelevu
kwa kushirikiana na Serikali ulianzisha Mabwawa 12 ya samaki (12000Vifaranga
vya samaki) 2021 lakini hivi tunavyoongea mkoa wa Iringa una mabwawa 52 ya
samaki(31840).
Kwa upande mazao Lishe (Mahindi Lishe,Maharage Lishe na
Viazi) mwamko kwa wakulima umekuwa mkubwa sana mfano kuna kata inaitwa Nyanzwa-Kilolo
Mradi wa Lishe Endelevu ulitoa mbegu za kutosha eneo
la robo ekari 2020 lakini mpaka kuna zaidi ya Ekari 17 ambazo zinalimwa Viazi
Lishe ambavyo ni kwa ajili ya kuboresha hali ya Lishe lakini pia kama chanzo
mbadala cha kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Ukilinganisha na awali ulaji wa mazao mchanganyiko
na mazao mchanganyiko umeongezeka sana kwenye maeneo yote ya utekeleza wa
Mradi.
Alisema mradi haukuishia kwa wakulima kwani ulifanya pia kazi ya
kuvijengea uwezo Vikundi 99 vya kuweka na Kukopa(VSLA) ili viwe na sifa ya
kupesheka na tayari 50 kati yake vimefanikiwa kupata mkopo wa Sh Milioni 83 ili
kuendelea kukuza shughuli zao za kijasiriamali.
“Mradi pia umedhamiria kuongeza upatikanaji na utoaji wa huduma
bora za lishe katika ngazi ya vituo vya afya na jamii kwa kuimarisha uwezo wa
watoa huduma za afya,” alisema.
Katika kikao cha pamoja cha wadau kilicholenga kujua mafanikio
ya utekelezaji wa mradi huo, changamoto na utatuzi wake ili kuweka mikakati
endelevu,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi
Leonard Masanja aliwataka viongozi na watendaji wa mkoa kushirikiana na wadau
ili kupunguza udumavu mkoani humo.
Mhandisi Masanja alisema;“Kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha
anatoa huduma bora za lishe na kuwafikia walengwa wote ili kupunguza athari za
utapiamlo na hasa udumavu miongoni mwa jamii yetu.”
Kwa kupitia msaada wa Watu wa Marekani, Masanja alisema mkoa wa
Iringa unatambua mchango mkubwa wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu wa mwaka 2018
hadi 2023 katika kutatua tatizo la lishe duni, utapiamlo.
Alisema mradi huo umechangia katika maeneo mengi yakiwemo;
kuongeza hamasa ya mabadiliko ya tabia kwa wanawake wajawazito, wanaonyonyesha,
watoto walio chini ya miaka mitano na vijana wa rika balehe kwa kupitia
wanawake vinara, vikundi malezi na klabu za lishe.
Eng. Masanja aliwataka viongozi na watendaji wa Mkoa wa
Iringa wameshauriwa kushirikiana katika kuhakikisha udumavu unapungua ili kuwa
na watoto wenye afya ya mwili na akili.
Alisema kuwa lishe ndiyo msingi wa maisha ya mwanadamu na
kuongeza kuwa afya ya mwanadamu ikiharikiwa kwa lishe duni katika siku elfu
moja (1,000)za mwanzo wa uhai, haziwezi kurekebishika kwamwe katika maisha yote
ya mwanadamu.
Eng. Masanja alisema kila mmoja wetu anatakiwa kuhakikisha
kuwa anatoa huduma bora za lishe na kuwafikia walengwa wote ili kupunguza
athari za utapiamlo hasa udumavu
Pia aliwasihi viongozi kusimamia zoezi la mipango na
bajeti za lishe kwa mwaka 2023/24 kuanzia ngazi ya kijiji hadi halmashauri ili
kuhakikisha shughuli ambazo zimepangwa zinaendelea kutatua
changamoto zilizopo katika jamii.
“Vituo vyote vya kutolea huduma za afya,shule na serikali
mtambuka zipange shughuli za lishe zitakazosaidia kupunguza utapiamlo,”alisema
Masanja.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Lishe Endelevu
Tanzania Dk Joyceline Kaganda, Dk Benny Ngereza alisema mbali na Iringa, mradi
huo wa miaka mitano unatekelezwa katika mikoa ya Rukwa, Morogoro na Dodoma.
Dkt. Joyceline Kaganda, alisema kuwa lengo kubwa ya kikao
hicho ni kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi kwa miaka minne, hasa katika
mkoa wa Iringa.
Dkt. Ngereza aliwataka maofisa mipango, wahasibu na
maofisa lishe wa halmashauri kusimamia upangaji na utekelezaji wa shughuli za
lishe ili kupunguza changamoto za lishe duni.