Na Junior Mwemezi, TARI
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania -TARI imesema itaendelea na utaratibu wa kuwajengea uwezo
watumishi wake wa idara tofauti juu uandikaji wa maandiko ya miradi itakayoweza kuongeza ufanisi katika maswala
ya kiutafiti.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa TARI Dkt Joseph
Ndunguru katika kikao chake na watumishi wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha
Maruku mkoani Kagera ikiwa ni mwendelezo
wa ziara yake ya kikazi katika vituo vya ukanda wa ziwa.
Dkt Ndunguru amesema wafadhili wengi wamekuwa wakishindwa kutoa pesa katika
miradi mbali mbali kutokana na waandaaji wa maandiko ya miradi hiyo kutoainisha
mambo muhimu ,ambayo yanaweza kuwashawishi wafadili .
Aidha Dkt Ndunguru amewaeleza wafanyakazi wa TARI Maruku kuwa njia pekee ya kufikia mafanikio ni
kuepukabhana makundi,ubinafsi na kujenga umoja na kutambua wote wanajenga
nyumba moja ambayo ni Tanzania.
Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa TARI Dkt Joseph Ndunguru akizungumza na watumishi wa TARI wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku mkoani Kagera.
Watumishi wa TARI Kituo cha Maruku Kagera wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Watumishi wa TARI Kiruo cha Maruku wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.