Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikabidhi kiasi cha shilingi milion moja kwa viongozi wa timu ya mbugani FC
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akipokea mipira kutoka kwa kampuni ya CRJE (EAST AFRICA) LTD kupitia kwa Meneja mradi Zhang linjie kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo kufanya mazoezi
Wachezaji na wadau wa soka wa kata ya Mboliboli wakiwa kwenye hali ya furaha
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa sambamba na diwani wa kata ya Mboliboli na kaimu afisa tarafa ya Pawaga.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya Soka ya Mbugani Fc ya kata Mboliboli wilayani Iringa
imekabidhidhiwa kitita Cha shilingi milioni milioni Moja iliyotolewa na wadau
wa soka wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya kama sehemu ya pongezi baada ya kutwaa
ubingwa katika mashindano ya Mbomipa Cup.
Kiasi hicho Cha Fedha kimetolewa kupitia harambee
iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ambapo amewahimiza
wadau wa soka Wilayani Iringa kuisaidia Timu hiyo Ili kuiwezesha kutatua
Changamoto zinazoikabili ikiwemo ukosefu wa vifaa vya Michezo na fedha Kwa
ajili ya uendeshaji wa Timu hiyo.
Moyo amesema Timu hiyo imeonesha ukomavu Kwa kutwaa
ubingwa wa kombe la MBOMIPAkupitia Michezo iliyojikita katika kuhamasisha
Utunzaji wa Mazingira na uhifadhi wa Wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Sita
chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuchochea Ulinzi wa Wanyamapori
kwalengo la kuvutia watalii nchini
Katika Risala yake Kwa washiriki wa harambee hiyo wakiwemo
wachezaji wa Timu ya Mbugani Fc Mkuu wa Wilaya Iringa Mohamed Moyo amewataka
kuwa mabalozi wa uhifadhi Kwa kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu
wanafanya ujangiri katika hifadhi Ili kuwezeshabhatua za kisheria kuchukuliwa.
Katika hafla hiyo kampuni ya CRJE (EAST AFRICA) LTD
kupitia kwa Meneja mradi Zhang linjie ilichangua mipira miwili kwa ajili ya
kuiwezesha timu hiyo kufanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya kiwilaya na
mkoa.
katika halfa hiyo ya kuwapongeza mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo alifanikisha kuchangisha kiasi cha shilingi milioni moja
kwenye harambee waliyoifanya siku ya kuwapongeza.
Timu ya
Soka ya Mbugani Fc ya kata Mboliboli wilayani Iringa inakabiriwa na changamoto
ya ukosefu wa vifaa vya mazoezi kama vile jezi,bipsi,viatu vya wachezaji,vifaa
vya golikipa,koni,nyavu na mipira hivyo wamewaomba wadau mbalimbali kuwachangia
ili waweze kufikia malengo wanayoyakusudia.