Askofu wa kanisa la BCIC mbezi beach, Askofu Sylvester Gamanywa akiongea na waandishi wa habari leo kuhusu Tamasha kubwa la siku tatu(3) linaloanza leo tarehe 2 hadi trh 4 December.
Mtumishi wa kimataifa kutoka Canada Dr Peter Youngren.
………………………….
Mwinjilisti wa Kimatiafa Kutoka Nchini CANADA Dkt Peter Youngren amewasili nchini Tanzania kwa mara nyingine kwa ajili ya tamasha kubwa la siku tatu la uimbaji na Miujiza litakalofanyika katika kanisa la BCIC Mbezi Beach Jijini Dar es salaam linalongozwa na Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa.
Akizungumza mara baada ya kupokelewa Kanisani hapo Dkt Youngren amesema kuwa maombezi hayo yatalenga kuombea maisha ya Watanzania waliokumbwa na matatizo mbalimbali pamoja na kuliombea Taifa kutokana na kukumbwa na majanga mbalimbali yakiuchumi, Kisiasa na kijamii
Dkt Youngren amesema kwamba maombi hayo ya siku tatu ambayo yameanza leo Desemba 2 hadi 4 yatasaidia kuwaondolea changamoto mbalimbali Watanzania wenye changamoto mbalimbali ikiwemo magonjwa,ukosefu wa Ajira,Ukraine pamoja na migogoro ya ndoa,inayowafanya wakate tamaa katika maisha yao.
“Kila wakati wa majanga ni fursa, Ulimwengu unakabiliwa na majanga , Uchumi kuporomoka haya yanatufanya sisi viongozi wa dini tufanye mambo mazuri zaidi katika maombezi yetu hivyo tunachohitaji ni ufahamu mpya katika wakati huu changamoto kwani ni mkakati za fursa ” alisema Dkt Youngren.
Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la BCIC Askofu Silvester Gamanywa amesema kwamba wanatarajia mabadiliko makubwa yakiroho na kiuchumi kupitia tamasha hilo la uimbaji na miujiza hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tamasha hilo.
“Maombi haya nikwajili ya kuombea jamii na Taifa kwa ujumla , tunatarajia matokeo makubwa, nawaomba watu wenye matatizo mbalimbali waje wapate huduma ya maombezi katika tamasha hili la historia” alisisitiza Askofu Gamanywa.