NA
MWANDISHI WETU
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetwaa Tuzo ya Umahiri
katika Uwasilishaji wa Taarifa za
Mahesabu kwa mwaka 2021, kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Tuzo
hiyo iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania
(NBAA) imepokelewa na Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi katika
hafla iliyofanyika katika hotel ya APC Bunju jijini Dar es Salaam Jumatano usiku Novemba 30,
2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Ikulu, Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, CPA. Jamal Kassim Ali.
PSSSF
imetwaa tuzo hiyo ya umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2021
(Best Presented Financial Statements for the Year 2021 Awards) kwa mwaka wa
pili mfululizo.
Akizungumza
kufuatia ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba alisema , tuzo
hiyo itaongeza chachu kwa watumishi wa PSSSF katika kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia weledi na hivyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wa Mfuko.
Aidha
Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Bi. Beatrice Musa-Lupi alisema ushindi huo ni ishara ya kwamba PSSSF inaandaa
mahesabu kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa lakini pia inaashiria
uwepo wa weledi wa tasnia husika kwa upande wa watumishi.
“Sambamba
na hayo niliyoyasema pia inaashiria uwepo wa usimamizi makini wa fedha za
wanchama na hii inatupatia heshima kama
taasisi.” Alisema Mkurugenzi huyo wa Fedha PSSSF.
Aliwahakikishia
Wanachama dhamira ya PSSSF ya kuhakikisha
usalama wa michango yao unazingatiwa kwa kiwango cha juu wakati wote, ikiwa ni
pamoja na kuwepo uwazi kwenye usimamizi na utunzaji wa rasilimali za Mfuko.
“Ushindi
huu pia unaashiria uwepo wa kesho ya wanachama wetu kama kaulimbiu yetu
inavyosema Leo. Kesho. Pamoja.”
Alihitimiaha Bi. Beatrice Musa-Lupi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais-Ikulu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Jamal Kassim Ali
(Kushoto) akimkabidhi tuzo ya Umahiri katika uandaaji na uwasilishaji taarifa
za fedha kwa mwaka 2021, Mkurugenzi wa Fedha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa
Watumishi wa Umma (PSSSF), Beatrice Musa-Lupi wakati wa kilele cha miaka 50 ya
Boadi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Maheabu Tanzania (NBAA) kilichofanyika hoteli
ya APC Bunju jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Desemba 1, 2022.