Mtaalamu wa zao la pamba kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP,) Joelcio Carvalho akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Nguge kilichopo Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza namna ya kutumia teknolojia ya kuchanganya udongo kwa kutumia mashine maalumu wakati wa mafunzo kwa vitendo kupitia mradi wa Beyond Cotton unaofadhiliwa na Serikali ya nchi ya Brazili kwa kushirikiana na Tanzania chini ya WFP, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) na Bodi ya Pamba (TCB) unaolenga kuinua tija ya zao la pamba kwa wilaya za Magu, Kwimba na Misungwi mkoani hapa. Katikati mwenye kofia ya blue anaye shuhudia mafunzo hayo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo akijifunza kutumia mashine maalumu ya kuchanganya udongo wakati wa mafunzo hayo.
Mkulima wa Kijiji cha Nyashani Kata ya Mwaniko, Hellena Mane (70) akijifunza kutumia mashine maalum ya kuchanganya udongo wakati wa mafunzo hayo.
Mratibu wa zao la pamba nchini Dk. Paul Saidia alitoa hamasa kwa wananchi wakati akishiriki utekelezaji wa mradi huo. Kata ya Nguge wilayani Misungwi mkoani hapa.Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Misungwi, Dk. Chrispine Shami akizungumza na wakulima wakati wa mafunzo hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu.
Ujenzi wa tenki la kuvunia maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji linalojengwa Shule ya Msingi Nguge ukiendelea.
Mtaalamu wa zao la Pamba kutoka WFP, Joelcio Carvalho akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Nguge kilichopo Kata ya Mwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza namna ya upandaji mbegu za pamba kwa kuzingatia vipimo.
Mtaalamu wa zao la pamba kutoka WFP, Joelcio Carvalho akiwaelekeza wakulima wa Kijiji cha Nguge kilichopo Kata yaMwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza namna bora ya kupima hali ya hewa kwa kutumia kifaa maalumu cha kupima kiasi cha mvua kabla ya kupanda pamba maarufu ‘rain gauge’Mratibu wa Lishe kutoka Wizara ya Kilimo Magreth Matai akitoa mafunzo kwa akinama wa Kata ya Nguge kupitia mradi huo.
Mtaalamu Mwandamizi wa masuala ya lishe na virutubishi kutoka TARI Ukirigulu Dk. Calesma Chuwa akisimamia utekelezaji wa mafunzo kupitia mradi wa ‘Beyond Cotton’ kwenye eneo la kuboresha lishe kwa wakulima wa kata hiyo..