Watumishi wa Mahakama za Wilaya mpya nchini zilizozinduliwa hivi karibuni wanaendelea kupatiwa Mafunzo ya Huduma kwa mteja longo likiwa ni kuboresha utendaji kazi katika Mahakama hizo ili wananchi waweze kupata huduma bora ya utoaji haki.
Tarehe 25 Novemba, 2022 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alizindua Mahakama ya Wilaya Busega iliyowakilisha Mahakama nyingine mpya za Wilaya mpya 17, Mahakama hizo zilizojengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia ni pamoja na; Butiama, Rorya, Songwe, Gairo, Mkinga, Mvomero, Kilombero, Mbogwe, Nyang’hwale, Kyerwa, Itilima, Missenyi, Kaliua, Uvinza, Buhingwe, Kakonko na Tanganyika.
Katika siku ya tatu ya Mafunzo hayo; Mada zilizotolewa ni pamoja na; Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania na ya Mabadiliko ya kiutendaji (Change Management).
Yafuatayo ni matukio katika picha ya Watoa mada mbalimbali waliotoa mada siku ya tatu (3) ya mafunzo hayo:-
Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso akiwasilisha Mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania kwa Watumishi wa Mahakama mpya za Wilaya. Bw. Uisso amesisitiza Watumishi hao kuwa sehemu ya utekelezaji wa Mpango mkakati huo ili kuendeleza uboreshaji wa huduma na hatimaye wananchi wapate huduma ya haki kwa wakati.
Muonekano wa sehemu ya wasilisho la Mpango Mkakati lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji-Mahakama ya Tanzania, Bw. Erasmus Uisso (hayupo katika picha).
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo wa Huduma kwa mteja ambao ni Watumishi wa Mahakama mpya za Wilaya wanaopata Mafunzo kwenye ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Morogoro wakifuatilia kwa makini mada inayotolewa.
Mwezeshaji akiendelea kutoa Mada kwa Washiriki wa Mafunzo (hawapo katika picha).
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Andrew Msami akiwasilisha mada ya Mabadili ya kiutendaji (Change Management) kwa Washiriki wa Mafunzo ya huduma kwa mteja yanayotolewa kwa Watumsihi wa Mahakama mpya za Wilaya.
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo wakifuatili mada inayotolewa.
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Andrew Msami akiendelea kuwasilisha mada, amewasisitiza watumishi kuwa chanzo cha mabadiliko kwa kuwa na mtazamo chanya (positive attitude) ili kuweza kufanya kazi zitakazoleta matokeo chanya.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama-Morogoro)