Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha leo.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya udhibiti Huduma za Nishati na Maji Kanda ya Kaskazini Injinia Lorivii Longidu akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo jijini Arusha.
*********************
JULIETH LAIZER,Arusha
Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda amewataka watoa huduma wa Tanesco na Auwsa kutambua wajibu wao kuwa wana haki ya kuwapokea wananchi kwa ukarimu na kusikiliza kero zao za huduma ya nishati na maji.
Mtanda ameyasema hayo wakati akifungua semina ya kuwaelimisha madiwani wa jiji la Arusha majukumu ya Ewura juu ya uthibiti wa huduma za nishati na maji.
Amesema kuwa, ni wajibu wa Tanesco na Auwsa kutambua kuwa ni wajibu wao kuwahudumia wananchi pindi wanapofika katika ofisini zao sambamba na kuwatatulia kero zao kwa wakati.
“Naipongeza Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji Ewura Mkoa wa Arusha kwa kuandaa mafunzo kwa madiwani wa Jiji la Arusha pamoja na watendaji wa kata wote kwa pamoja kuelimishwa kazi za Ewura kwaji hawa ndio wanajua changamoto wanazokabaliana nazo wananchi”amesema.
Mtanda amesema kuwa mkutano huo umelenga kujadili kero mbalimbali zitokanazo na sekta ya maji ,umeme ambayo ndio matumizi makubwa kwa wananchi ya kila siku ambapo wananchi wengi watahitaji kutambua huduma wanazo pata kama ni sahihi .
Amesema kuwa madiwani na watendaji wa kata wana nafasi kubwa katika kuwafikishia wananchi ujumbe juu ya huduma wanazo zipata kutoka katika mamlaka ya maji pamoja na Tanesco kwa kutambua huduma wanazo zipata ni sawa na kile wanacho lipia kwani kumekuwepo na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi juu ya bili za maji kuwa kubwa ikilinganishwa na matumizi yao .
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA)Kanda ya kaskazini,Injinia Lorivii Long’idu amesema kuwa wao kama Mamlaka wameona nafasi kubwa waliyonayo katika jamii ni vyema kushirikishwa kutambua kazi za mamlaka pamoja na kusaidia kuelimisha wananchi juu ya changamoto wanazo kutana nazo katika huduma za maji na umeme .
Amesema kuwa ,mpaka sasa wamefanikiwa kutatua malalamiko ya wananchi waliofikisha ofisini kwao kwa mwaka wa fedha wa 2021 /2022 zaidi ya changamoto 1500 ambazo zimefanyiwa kazi na wananchi kurejeshewa majibu hususani malalamiko ya matumizi ya ankara za maji kuwa juu .
Longi’du amewataka wananchi wanao kutana na changamoto za kupandishiwa gharama za matumizi ya maji au nishati ya umeme kupanda kwa unit bila kuwepo na taarifa rasmi kufika ofisini kwao na kutoa malalamiko yao na kuweza kutatuliwa kwa wakati.
Amesema kuwa, mamlaka hiyo iko kwa ajili ya kutatua changamoto na kuwaelimisha wananchi luhusu huduma ambazo wamekua wakizipata kutoka tahasisi za Mamlaka za maji na Umeme ambazo ndio tahasisi kubwa zinazo wafikia wananchi mara nyingi .
Meya wa Jiji la Arusha ,Maxmalian Iraghe amesema kuwa na Madiwani kwa pamoja wamesema mkutano huo umekuwa chachu ya kutatua changamoto za wananchi wao na kuwa watakuwa mabalozi wazuri kufikisha ujumbe kwa wananchi ambao wamekuwa wakiwatumikia latika kata zao na watashirikiana na watendaji wa kata kuwafikia wananchi .