NAIBU Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais TAMISEMI Ramadhan Kailima,akizungumza wakati wa kongamano la 14 la wanataaluma la Chuo cha Serikali za Mitaa (HOMBOLO) ikiwa ni maandalizi kuelekea Mahafali ya 14 ya Chuo hicho.
KAIMU Mkuu wa Chuo cha Hombolo Dk. Mashala Lameck ,akizungumza wakati wa kongamano la 14 la wanataaluma la Chuo cha Serikali za Mitaa (HOMBOLO) ikiwa ni maandalizi kuelekea Mahafali ya 14 ya Chuo hicho.
Naibu Mkuu wa Chuo,Taaluma,Utafiti na Ushauri Dokta Michael Msendekwa,akizungumza wakati wa kongamano la 14 la wanataaluma la Chuo cha Serikali za Mitaa (HOMBOLO) ikiwa ni maandalizi kuelekea Mahafali ya 14 ya Chuo hicho.
SEHEMU ya washiriki pamoja na Waandihsi wa habari wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais TAMISEMI Ramadhan Kailima (hayupo pichani) wakati wa kongamano la 14 la wanataaluma la Chuo cha Serikali za Mitaa (HOMBOLO) ikiwa ni maandalizi kuelekea Mahafali ya 14 ya Chuo hicho.
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
WAKURUGENZI nchini wametakiwa na utaratibu maalum wa kuwatambua na kuwabaini wafanyabiashara wanaouza bidhaa katika maeneo ya shule ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 30,2022 jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais TAMISEMI Ramadhan Kailima katika kongamano la 14 la wanataaluma la Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI)ikiwa ni maandalizi kuelekea Mahafali ya 14 ya Chuo hicho yanayofanyika ambapo watahitimu wanachuo 4923.
Amesema hivi karibuni kumeripotiwa uwepo wa vyakula ambavyo vingi ni vile vinavyopendwa na watoto kutengenezwa na dawa za kulevya hivyo wakurugenzi washirikiane na kamati za shule kuwatambua wafanyabiashara wa maeneo hayo.
Aidha amewataka wakurugenzi wote nchi nzima kwa kushirikiana na kamati za shule waangalie na watafakari namna ya kuwatambua na kuwabainisha wafanyabiashara wote wenye vitendo hivyo.
“Wanauza pipi na zile biskuti nitumie fursa hii kuwaasa wakurugenzi wa halmashauri wote kwamba wale wanaoenda kuuza pipi kwenye maeneo ya shule zetu watafute namna ya kuwatambua hao watu kwa kujua uhakika wao hao wauzaji tunawajua wanatoka wapi mitaa na vijiji wanavyotoka tuwajua ili isaidie kufukuza janga hilo,
“Ni hatari kwasababu akianza kutafuna ile pipi kwa mara ya kwanza atajisikia vizuri baada ya muda anajisikia kuumwa kwasababu ya pipi ya mia moja,mia mbili,”amesema Kailima.
Hata hivyo ,Kailima amekitaka chuo hicho kufanya utafiti ili kubaini sababu za baadhi ya hoja za halmashauri kujirudia katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
”Nataka Muandae mafunzo kwa viongozi wanaochaguliwa na kuteuliwa wakiwemo madiwani ili kuondoa migogoro inayotokea katika baadhi ya maeneo inayosababishwa na baadhi ya viongozi kutojua mipaka ya majukumu yao.”amesema
Kongamano hilo limebeba mada isemayo Mchango wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kufikia dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2022.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo Dk. Mashala Lameck amesema wameweka mada hiyo kwa kuwa wanalo jukumu kama chuo la kuhakikisha dira hiyo inafikiwa.
“Tutawasilisha mada na wanataaluma watachangia na sisi kama chuo tunaowajibu sasa kufikia dhira hiyo kupitia shughuli zetu tunazozifanya sisi ambazo ni mafunzo kupitia huduma za ushauri lakini tunafanya haya yote katika Serikali za mitaa tukiamini sisi tunawajibu na tumepewa jukumu na Serikali la kuwa chuo kiongozi cha mafunzo yanayoendeshwa katika Serikali za mitaa.
Awali,Naibu Mkuu wa Chuo,Taaluma,Utafiti na Ushauri Dokta Michael Msendekwa amesema kama chuo wanajivunia kutoa wahitimu wanaokodhi soko la ajira.
Dkt.Msendekwa amesema kuwa wamepokea maagizo waliyopewa kuhusu madawa ya kulevya,kuwa mafunzo viongozi wa serikali za mitaa pamoja na kufanya utafiti wa hoja za Mkaguzi mkuu wa serikali na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI na watayafanyia kazi.
“Tumelipokea hilo tutaendelea kulifanyia kwa weledi tunayo huwa tunafanya kwasababu ni msisitizo tutaendelea sasa lakini ameongea mengi kuna watumishi pia hawa watendaji wa vijiji,kata na mitaa lakini kwenye vitongoji pia kuna wenye viti pia hawa wawezekupatiwa mafunzo mara kwa mara na chuo cha serikali za mitaa,”amesema Dkt.Msendekwa.