MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo ,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba jijini Dodoma.
MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo,akifafanua mambo mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba jijini Dodoma.
…………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Bw.Sosthenes Kibwengo,amesema kuwa wameanza kufuatilia zoezi la ugawaji pembejeo za kilimo zenye ruzuku ili kuzuia vitendo vya ubadhilifu.
Kibwengo ameyasema hayo leo Novemba 29,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wameamua kufuatilia ili kuhakikisha lengo la Serikali linatimi.
Kibwengo amewataka watakaohusika na mchakato wa ugawaji wa pembejeo hizo kuzingatia taratibu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote watakaohusika na ufujaji.
“Huko nyuma kulikuwa na udanganyifu katika zoezi la ugawaji wa pembejeo za kilimo zilizokuwa na ruzuku hadi kusababisha kufunguliwa mashauri ya jinai mahakamani dhidi ya baadhi ya watendaji na mawakala wa pembejeo za kilimo, tumeanzisha ufuatiliaji kwa mwaka huu ili kuhakikisha lengo la serikali linatimia”amesema Kibwengo
Hata hivyo kibwengo amesema katika kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu wamefanikiwa kurejesha sh.milioni 75.5 zilizokuwa mikononi mwa mawakala wanaotumia mashineza kielekroniki kukusanya mapato na kuziwasilisha benki.
Amesema wanaendelea kushirikiana na halmashauri za mkoa wa Dodoma kuhakikisha ushuru na tozo zinazokusanywa kwa njia ya mashine zinawasilishwa benki kwa wakati.
”Tumefuatilia miradi 31 ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 19.98 katika sekta za umwagiliaji,maji,afya,elimu na ujenzi ambapo mapungufu bainishwa yalirekebishwa na sh.milioni 266.5 ambazo zililipwa bila kazi zinafuatiliwa.
Aidha Kibwengo ameeleza mikakati ya TAKUKURU katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka huu ni kuelimisha wananchi ili kuhamasisha ushiriki wao katika kuzuia rushwa kwa kuongeza vipindi vya uelimishajikwa njia ya redio.
Ametaja mkakati mwingine kuwa ni kuchochea uitishaji wa wananchi kwenye mikutano ya kisheria ya mitaa,vijiji na kuelimisha wananchi katika mikusanyiko mbalimbali hasa maeneo ya pembezoni.
“Tutaelimisha kamatiza ujenzi, manunuzi na kauzi za miradi ya maendeleo ili wazingatie sheria na kanuni za manunuzi kwa umma.
Ameongeza:”TAKUKURU itaendelea kufuatilia uwasilishaji kwa wakati fedha zinazokusanywa kwa mashine za kielektroniki ili kuzuia ubadhilifu na kuhamasisha fikra kupitia kundi la vijana kwamba kuzuia rushwa ni jukumu la kila mmoja.