Mmoja wa Shujaa kutoka Taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) akitolewa damu kwa ajili ya kuchangia akiba ya damu wakati Mashujaa kutoka SMAUJATA walipotembelea Hospitali ya Makiungu iliyopo wilayani Ikungi kwa ajili ya kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili, pamoja na kuwajulia hali wagonjwa ambapo pia walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo katika ziara iliyofanyika jumamosi..
Uchangiaji wa damu ukifanyika.
Mashujaa wakifanya usafi kuzunguka viunga mbalimbali vya Hospitali hiyo.
Usafi ukiendelea.
Mashujaa wa SMAUJATA wakiwafariji wagojwa kwa kufanya maombi pamoja.
Sabuni zikitolewa kwa wagonjwa.
Picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MILA na desturi na ukosefu wa elimu vimetajwa kuwa sababu ya kuwepo kwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii kwa watoto ikiwa ni pamoja na
kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wadogo.
Sababu hizo zimetolewa na wananchi wa Wilaya ya Singida na Iikungi wakati
Taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania –( SMAUJATA) wakito elimu ya kupinga vitendo vya ukatili
wa kijinsia kwa akina mama wajawazito katika Hosiptal ya Makiungu wilayani Ikungi..
Wamesema kuwa kuna baadhi ya wananchi bado wanaendelea kufuata mila na
desturi zilizopitwa na wakati ambazo bado zinasababisha kufanyika kwa vitendo
hivyo vya ukatili.
Wameongeza kuwa hata mangariba wamebadili njia ya kufanya ukeketaji ambapo
kwa sasa vitendo vya ukeketaji unafanywa kwa watoto wachanga .
Kutokana na sababu hizo, taasisi ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii
tanzania – SMAUJATA imeitembelea hospital ya makiungu wilayani ikungi mkoani singida kutoa elimu ya kupambana na
ukatili wa kijinsia hasa vitendo vya ukeketaji kwa watoto kwa akina mama
wajawazito.
Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Singida Dismas Kombe, alisema wanatoa elimu
kwa akina mama wajawazito kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua ubaya wa
ukatili wa kijinsia ili waweze kuwalinda watoto wao wanaotarajia kuwaza na
vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.
Kombe alisema kuwa bado makundi la watoto na wanawake yanafanyiwa vitendo
vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ukeketaji kwa watoto, vipigo na
ubakwaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Kombe ameongeza pia changamoto iliyopo kwa jamii ni kushindwa kuripoti
vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa akina mama na watoto, kutokana
na vitendo vingi kufanywa na wanandugu.
Katibu idara ya wanaume SMAUJATA – Mkoa Singida, Simon Mdumah alisema kundi la wanaume nalo ni moja
ya kundi linalofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa sasa, changamoto ni
namna ya wanaume hao kuripoti vitendo hivyo wanavyofanyiwa.
Mdumah alisema wanaume wengi wanashindwa kuripoti ukatili wanaofanyiwa
kutokana na mila na desturi za kiafrika na kuogopa kuonekana wadhaifu kwa wake
zao na jamii kwa ujumla.
Pamoja na kutoa elimu, SMAUJATA pia imefanya usafi katika hospitali hiyo na
kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wale wenye uhitaji wa damu.