********************
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania ambaye pia ni Kada mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mwl.Mohamed Mwampogwa maarufu ‘Mwalimu Pogwa Mzalendo tz’ ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita iliochini ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana ambayo inafanya ya kutoa huduma bora kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa Uhuru kwa Wananchi na Vyombo vya habari katika kutoa maoni,kukosoa na kuishauri Serikali na kusema kuwa hii ni hatua nzuri sana inayo ashiria Utawala bora kwa taifa.
Mwl.Mwampogwa ambaye ni Muasisi wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania lenye Wanachama karibia 125000 inchini mbalo limejikita katika kutoa Elimu na Hamasa juu ya Agenda ya Uzalendo kwa Jamii amewataka Wajumbe wa Jukwaa hilo kuongeza kasi ya kutoa Elimu ya Uzalendo kwa Jamii hususan maeneo ya Vijijini ambako baadhi ya Wananchi hawatumii Mitandao ya Kijamii lakini pia amewataka Wajumbe wa Jukwaa hilo kuongeza kasi ya kuzitafsiri na kuzitangaza kazi zote zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Chama na Serikali bila kusahau kukosoa na kuishauri Serikali kuwa nini kifanyike ili kwa pamoja tulijenge taifa letu kwa Amani na Upendo.
Mwl.Mwampogwa amewaelekeza Wenyeviti na Makatibu wa Majukwaa hilo katika ngazi ya Wilaya na Mikoa kuhakikisha kuwa wanawaongoza Wajumbe wa Majukwaa yao vyema kwa kuweka Program maalumu za kuyagusa makundi maalumu kama Yatima,Walemavu,Wazee,Wajane na Watoto Wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia misaada pamoja na kuihamasisha Jamii kutoa msaada na haki za msingi za makundi hayo ambayo yanaitegemea Jamii yao.
“Katika kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia Wajumbe wa Jukwaa la Wazalendo huru wanapaswa wajitahidi kuvipinga vitendo hivyo na pia kutoa Elimu kwa Jamii juu ya madhara yanayo ikumba Jamii kutokana na hali hii ya Ukatili lakini pia kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa taarifa za Ukatili wa Kijinsia na kuhusu suala la kukabiliana na hali ya tabia nchi Majukwaa ya Wazalendo huru ngazi ya Wilaya na Mikoa yaendeshe Program za kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu ya umuhimu wa kupanda” alisema Mwl.Mwampogwa.
Mwl.Mwampogwa ambaye pia ni Msanii wa Muziki wa nyimbo za Asili,Uzalendo na Kizazi kipya nchini amehimiza Wazalendo huru Tanzania kutumia Sanaa mbalimbali kutoa Elimu ya Uzalendo mfano nyimbo zinazotoa Hamasa ya kutunza Amani na Utulivu,Mazingira nk lakini pia kutoa Elimu ya Ulipakodi,Ulinzi wa Rasilimali za taifa,Usalama Barabarani nk.Lakini pia amesisitiza Wazalendo kuungana na kuandika Vitabu vya Mashairi na Tenzi kama sehemu ya kukuza Lugha yetu ya Kiswahili na pia kulinda Utamaduni wetu nchini.Hata hivyo tarehe 20 April 2022 Mwalimu Mwampogwa anatarajia kuzindua kitabu chake cha Mashairi kiitwacho “Diwani ya Mwalimu Pogwa Mzalendo”.