Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Ruaha (CDTI, Godfrey Mafungu akiongea na wahitimu pamoja na wageni waalikwa juu ya maendeleo ya chuo hicho
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHUO cha Maendeleo ya Jamii Ruaha
(CDTI) kilichopo mkoani Iringa kimeanza Kutekeleza taratibu za awali za
kufanya utafiti wa hali ya Lishe na Udumavu katika Manispaa ya Iringa na
kimeanzisha Dawati la Jinsia kwa ajili ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia lengo
likiwa ni kupunguza udumavu na kuondoa ukatilii kwa jamii.
Akizungumza
wakati wa mahafali ya chuo Maendeleo ya Jamii Ruaha (CDTI,mkuu
wa chou hicho Godfrey Mafungu alisema kuwa chuo hicho kimefanikiwa
kujenga ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanachuo 260, Mabweni
mawili yenye uwezo wa kuchukua wanachuo 128 na maktaba yenye uwezo wa kuchukua
wanachuo 144 kwa awamu moja
Mafungu alisema kuwa wameanza utekelezaji wa programu ya
Ushirikishwaji jamii,Uanagenzi na kituo cha ubunifu na maarifa ikiwa ni
utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ibara 229 na uwepo wa miradi ya
uzalishaji mali kwa lengo likiwa ni kutoa mafunzo na kuongeza mapato ya ndani
ya Chuo.
Alisema kuwa katika kuendelea kuboresha miundombinu ya chuo ili kuwezesha
kutoa huduma bora za mafunzo kwa wanachuo,serikali kupitia Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum ilikipataia chuo kiasi cha shilingi
za kitanzania milioni mia sita (600,000,000.00) kuweza kutekeleza miradi ya ujenzi
wa majengo manne.
Mafungu alisema kuwa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara (Lecture
Hall) unaogharimu shilingi za
kitanzania milioni mia moja (100,000,000.00) mpaka kukamilika
kwake na ina uwezo wa kuchukua wanachuo 260 kwa awamu moja, Ujenzi wa Maktaba
ya kisasa unagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia mbili
(200,000,000.00) na kuwa na uwezo wa kuchukua wanachuo 144 kwa
awamu moja na Ujenzi wa mabweni mawili unagharimu kiasi cha
shilingi za kitanzania milioni mia
tatu (300,000,000.00) ikiwa shilingi milioni mia moja hamsini (150,000,000.00)
kwa kila moja na uwezo wa kuchukua wanachuo 128 kwa awamu moja kwa majengo yote
mawili.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika mahafali hayo Naibu Waziri Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,wanawake na makundi maalumu Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amepongeza
chuo Cha maendeleo ya Jamii Ruaha mkoani Iringa Kwa mapambano dhidi ya udumavu
na utapiamlo.
Akitoa pongezi hizo Leo wakati wa Mahafali ya 14 ya chuo hicho
Naibu Waziri huo amesema jitihada kubwa zimefanywa na chuo hicho Katika utoaji
elimu ya lishe Kwa jamii inayozunguka.
Hata hivyo amepongeza menejimenti ya chuo Kwa kuendelea
kuimalisha Mapato ya ndani Kwa kubuni vyanzo vya Mapato kama ugugaji samaji,uchakataji
ngozi na shughuli nyingine za Kiuchumi.
Alisema alipofika chuoni hapo alitembelea mabwawa ya samaki na
kuona jitihada hizo kubwa ambapo kupitia ugugaji huo wananchi watapata Afya
Bora.
Aidha waziri Khamis alipongeza
chuo Kwa kupata kibali Cha utafiti wa lishe Iringa na kuagiza vyuo vingine
kuandika maandiko ya kazi mbali mbali za chuo Kwa lengo la Kutangaza chuo.
Akielezea changamoto za chuo hicho kama Nyumba za walimu na
Mabweni alisema changamoto hizo amezichukua na atakwenda kuzifanyia kazi kwa
kuwa suala la miundo mbinu ya barabara atauagiza uongozi wa mkoa ili kuboresha
mazingira ya chuo hicho.
waziri Khamis aliwataka wahitimu wa chuo
hicho kutumia vema mafunzo ambayo wamepata Kwa kwenda Vijijini kuwatumikia
wananchi kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan ameunda wizara ya
maendeleo ya Jamii ili kusaidia jamii kupata elimu Bora .
“Ndugu wahitimu mtakapopata fursa ya kupata kazi jiepusheni
na vitendo vya Rushwa na miawe mabalozi mazuri wa kutokomeza vitendo vya
ukatili wa kijinsia”
“Tumekuwa tukifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na
nimekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Chuo katika utekelezaji
wa majukumu yake, ninaahidi kutimiza wajibu wangu nikiwa kama Naibu Waziri, kwa
kutoa msaada pale itakapohitajika na nitakapoona inafaa”.
Alisema anatambua kuwa ili kuweze kufikia malengo waliyojiwekea
katika kutekeleza mpango mkakati wa Chuo, ni lazima kuwe na juhudi za makusudi
za kuhakikisha upatikanaji wa fedha za maendeleo.
” Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kwa kushirikiana na
Wizara yetu pamoja na Wizara ya Fedha kuhakikisha suala la upatikanaji wa fedha
za kutosha za ruzuku na miradi ya maendeleo kwa ajili ya uendeshaji wa Chuo
hiki linapewa kipaumbele Ndugu Wahitimu, Napenda nitumie fursa hii kuwapongeza
sana wote ambao mtatunukiwa hivi punde Stashahada na Astashahada za Maendeleo
ya Jamii. Niwapongezeni sana kwa juhudi kubwa mliyoonyesha katika kipindi chote
mlichokuwa hapa Chuoni,kilichowapelekea kufikia mahafali ya siku ya leo”
Alisema anatambua umuhimu wa elimu ya Maendeleo ya Jamii katika
maendeleo ya ulimwengu wa sasa; napenda niwasisitize umuhimu wa kujiendeleza
katika fani hii ili muweze kuwa chachu ya mabadiliko chanya ya kimtazamo wa
jamii.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anachukizwa Sana na vitendo
vya ukatili vinavyojitokeza Katika jamii yetu hivyo ni jukumu lenu kwenda
kulifanyia kazi janga la ukatili Kwa kutoa elimu Bora na wale wanaopata msongo
wa mawazo Kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili mkawasaidie kuwapa elimu.