Na. Damian Kunambi, Njombe.
Kutokana na Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kutosikika radio yoyote na kupelwkea kukosa taarifa mbalimbali za msingi Naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari ameitaka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania kutoa reseni kwa redio za Halmashauri zinazotaka kuanzishwa ili kuweza kupanua wigo wa kuhabarisha Umma hasa kwa maeneo ambayo hayafikiwi huduma .
Naibu waziri ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya mawasiliano ya simu wilayani Ludewa mkoani Njombe na kuongeza kuwa katika Halmashauri ambazo inavituo vya TBC na miundombinu yake inauwezo wa kutoa huduma vyema vinapaswa kuzisaidia Halmashauri katika kuweka booster kwenye minara yao ili wananchi waweze kuhabarishwa kupitia radio hizo za Halmashauri.
“TCRA hampaswi kufanya ukilitimba wowote juu ya kutoa Leseni kwa Halmashauri hizo ilimradi ziwe zimefuata sheria na kanuni zakuwawezesha wananchi hawa kuhabarishwa”. Amesema Eng. Kundo
Awali mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga aliwasilisha ombi hilo kwa Naibu waziri huyo na kusema kuwa wananchi wanahaki ya kuhabarishwa lakini kwa wilaya ya Ludewa imekuwa ni vigumu kupata taarifa kupitia redio hivyo Halmashauri hiyo tayari imekwisha andaa chumba cha studio na ili kuanzisha radio hiyo.
“Mimi na mkurugenzi wa Halmashauri tuliandika barua kuomba kuanzisha radio hivyo halmashauri itasaidiwa na serikali kupata redio hiyo na tayari kwa mwaka huu wa fedha mkurugenzi amekwisha tenga kiasi cha sh. Ml. 50 kwaajili ya kununua vifaa bidogo vidogo”. Amesema Kamonga.
Sanjari na hilo mbunge huyo pia amefurahishwa na ujenzi wa radio ya TBC ambayo jnajengwa katika kata ya Milo wilayani humo kwani aqali palikuwa na changamoto ya umeme hivyo kwa sasa changamoto hiyo imetatuliwa baada ya serikali kutoa kiasi cha sh. Ml. 480 kwaajili ya kutoa umeme katika kata ya Ludende na kuupeleka katika ofisi hizo.
“TANESCO wamekwisha anza kutengeneza njia za umeme toka wiki iliyopita huku nguzo zikiwa njiani kwaajili ya kuunganisha umeme huo”. Amesema Kamonga.